CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT,) kimeadhimisha Kongamano la nane la Wahitimu na kubainisha malengo yake ya ushindani katika kuwandaa wanafunzi wenye ujuzi na ubunifu watakaoweza kutengeneza ajira kupitia fursa mbalimbali ambazo Serikali imezitangaza ikiwemo uchumi wa Buluu, ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga Tanzania.

Akizungumza katika kongamano la nane la Wahitimu la chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT,) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC,) Abdi Mkeyenge amesema kongamano hilo limewakusanya pamoja na kujadili fursa na mikakati ya kukiendeleza chuo hicho kupitia fursa mbalimbali ambazo zimekiwa zikibainishwa na Serikali na taasisi ya sekta binafsi nchini.

Mkeyenge amesema, Ujuzi, Maarifa, tafiti na machapisho yanayochapishwa na chuo hicho ni nyenzo ya kukijenga chuo hicho ambacho kimeona fursa nyingi zikibainishwa na Serikali ambazo sekta ya usafirishaji inahusika moja kwa moja ikiwemo; ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, Tanzania, fursa za uchumi wa buluu, sekta ya usafirishaji wa anga na Ujenzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere fursa ambazo chuo hicho zimeona na zinafanyiwa kazi.

Mkeyenge amewashauri wahitimu kutumia ubunifu na maarifa waliyoyapata kwa kutengeneza ajira sio kutegemea kuajiriwa pekee.

"Ubunifu na kujizatiti kwa NIT katika masuala ya usafirishaji kunadhihirika wazi, nawasihi bunifu na maarifa mliyopewa msikae nayo mkayatumie kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla." Amesema.

Awali akizungumza katika Kongamano hilo Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Tanzania Prof. Zacharia Mganilwa amesema Kongamano hilo limelenga kuwakutanisha walimu, wanafunzi na wahitimu kwa kuwaonesha dira baada ya kuhitimu na namna ya kutumia maarifa waliyoyapata kwa vitendo kwa kujitengenezea ajira zao na kuajiri wengine.

Amesema chuo hicho kimejikita katika ushindani hasa kwa wakati huu ambao dunia ipo katika mageuzi makubwa ya kiuchumi na fursa nyingi katika sekta ya usafirishaji.

"NIT imekuwa ikiongeza ufanisi na kufanya tafiti mbalimbali ambazo zimekiwa zikiinua chuo hiki kwa kufanya vizuri katika wakati huu ambao ulimwengu unashuhudia mapinduzi makubwa ya teknolojia.'' Amesema.

Mganilwa amesema Kongamano hilo linawaweka pamoja wanafunzi, walimu na wahitimu na kujadili mabadiliko yenye tija kwa jamii pamoja pamoja na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao, kutoa zawadi kwa wastaafu waliotumikia chuo hicho kwa miaka 30 pamoja na kutoa zawadi kwa wakufunzi waliopata mafunzo ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema kuwa katika kongamano chuo hicho kimesaini hati ya makubaliano na kampuni ya Simba Logistics ambao ni wadau wakubwa wa usafirishaji na wamekuwa  wakitoa fursa ya walimu kujifunza kwa kutoa elimu ya nadharia na vitendo na kuwapokea wanafunzi kufanya mafunzo ya vitendo pamoja na kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao. 

Kongamano hilo limekwenda sambamba na kujadili mada mbalimbali huku wadau wakikakaribishwa kushiriki katika mchakato huo wa kukiendeleza chuo hicho.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC,) Abdi Mkeyenge akizungumza katika kongamano la nane la wahitimu la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT,) na kuwataka wahitimu hao kutumia vyema maarifa na ujuzi walioupata kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania Prof. Zacharia Mganilwa akihutubia katika hafla hiyo la kongamano la wahitimu wa chuo hicho na kueleza kuwa NIT inakwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia duniani na imekuwa ikiwaandaa wanafunzi kwa kuwapa ujuzi na maarifa leo jijini Dar es Salaam.














Matukio mbalimbali katika hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...