Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

MiCHUANO ya Kufuzu Kombe la Dunia kwa watu wenye wenye ulemavu inafikia tamati kesho kwa timu ya Ghana na Liberia kucheza mchezo wa fainali utakaopigwa Kesho katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mchezo huo wa Fainali ya Michuano ya Soka Afrika kwa watu wenye Ulemavu (CANAF) itawakutanisha timu hizo ambazo tayari zimeshafuzu kwenda Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Uturuki.

Ghana ilipata nafasi ya kufuzu fainali baada ya kushinda kwenye mchezo wa Nusu fainali dhidi ya Angola kwa magoli 3 - 0, huku Liberia ikipata nafasi hiyo baada ya kuwafunga Tanzania goli 1-0.

Mchezo mwingine wa hatua ya mshindi wa tatu itakuwa ni kati ya Tanzania dhidi ya Angola utakaochezwa kesho mapema kwenye uwanja huo.

Naye Rais wa Shirikisho la soka la wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi,amesema kuwa anamshukuru mungu kwa jambo la kujivunia licha ya kukosa matokeo mazuri na ni sehemu ya kujifunza.

Amesema kuwa Tanzania ilipata nafasi nyingi lakini ikishindwa kuzitumua kwa wakati, hivyo wapinzani wakatumia na kuibuka na ushindi .

" Wapinzani wetu wana uzoefu na wamechukua makombe matatu na tuangalie ,hivyo kwa muda uliobakia kocha ataweza kuyafanyia kazi mapungufu ikiwamo ya ushambuliqji na umaliziajikabla kuelekea kombe la Dunia," amesema Sarungi

Timu hizo zote zimefanikiwa kutinga kombe la Dunia 2022 nchini Qatar


 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...