MWENYEKITI wa Ushirika wa Chama cha kukopa na kuweka Akiba, Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP Benedict Wakuliyamba leo tarehe 21/12/1021 ametoa wito kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari Polisi wa Makao Makuu na Askari wa Jiji la Dodoma na aliwataka wanachama wa mfuko huo wa kuweka na kukopa wa Jeshi la Polisi (URA SACCOS) kuhakisha wanongeza Akiba zao na kununua hisa za kutosha ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika ukumbi wa Polisi Jamii uliopo mkoani Dodoma CP Wakulyamba amesema Chama cha Kuweka Akiba na Kukopa URA SACCOS kina wanachama wapatao zaidi ya 42.000 pamoja na matawi 7 nchini, huku akiwataka maafisa na askari ambao bado hawajajiunga waweze kujiunga kwasababu ni mfuko ambao una riba ndogo kuliko mifuko yoyote ya kuweka na kukopa.
Mwenyekiti wa Ushirika wa Chama cha kukopa na kuweka Akiba, Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP Benedict Wakuliyamba akizungumza katika ukumbi wa Polisi Jamii uliopo mkoani Dodoma leo Desemba 21,2021

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...