UMOJA wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT)Mkoa wa Njombe umefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika usimamizi wa miradi ya kiuchumi ya Chama hicho huku ukiahidi kuongeza kasi hiyo kwa ajili ya matokeo bora zaidi.

Akizungumza muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa cheti za pongezi kutokana na  ushindi huo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, katika Kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la UWT Taifa kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Scholastika Kevela alisema wao kama wanawake wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa huo, wamekoshwa na ushindi huo kwa kuwa umeonyesha kuwa mchango wao katika usimamizi wa miradi wa kiuchumi ya chama unaonekana.

"Sisi kama wanawake wa UWT wa Njombe tumefarijika  sana na ushindi huu na zaidi  umetupa  chachu ya kuendelea kuhakikisha  tunaongeza usimamizi wa miradi hiyo kwa ajili ya matokeo chanya ndani ya chama chetu" alisema Mama Kevela.

Aidha alisema malengo ya Umoja huo ni kuendelea kushirikiana kwa pamoja na kuweka mkazo katika usimamizi wa miradi hiyo na mingine ya kimaendeleo  inayotekelezwa na chama hicho kama moja ya majukumu yake.

Alisema usimamizi mzuri katika miradi hiyo ndiyo njia pekee itakayokiwezesha chama hicho kupiga hatua mbalimbali za maendeleo kutokana na umuhimu wake katika kuchangia mapato ya chama hicho.

Nafasi ya kwanza katika eneo la usimamizi wa miradi hiyo imechukuliwa na Mkoa wa Arusha, na na Mkoa wa Mwanza ukichukia nafasi ya pili huku yote ikipewa cheti cha pongezi kwa hatua hiyo.  

UWT mkoa wa Njombe pia imeushukuru uongozi wa UWT Taifa kwa kutambua juhudi wanazozifanya na kutambua mchango wao huku ikiahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kukikuza chama hicho.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa UWT mkoa wa Njombe amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan kulitumikia Taifa.

" Tupo naye na tutaaendelea kumuunga mkono kwa vitendo katika harakati zake za ujenzi wa Taifa tukizidi kusisitiza kuwa kazi iendelee kama anavyosisitiza" aliongeza Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Njombe Scholastika Kevela.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...