Na John Walter-Babati
Kituo cha kulea watoto wadogo cha Enhakore Day Care kilichopo Mtaa wa Negams Mjini Babati, kimefanya mahafali ya kwanza kuwaaga wanafunzi 14 waliohitimu elimu ya awali mwaka 2021, ambao wataingia darasa la kwanza mwaka 2022 katika shule mbalimbali za msingi .
Mahafali hayo yamefanyika kituoni hapo na kuhudhuriwa na wazazi ambapo mgeni Rasmi Selina Bukhay amewaasa wazazi na walezi waendelee kuwalea vyema watoto hao kama walivyokuwa kituo kilivyokuwa kikiliwalea vizuri na kwa maadili mema, huku akiwataka wapunguze ubize wa maisha na kuwalea watoto kwa kuhakikisha wanapata elimu bora ambayo ndiyo urithi katika maisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha ENHAKORE DAY CARE, Mchungaji Ezekiel Sabaya Laizer aliwapongeza wazazi kwa kuendelea kuwa na ushirikiano na walimu, ambapo ndiyo moja ya siri ya mafanikio ya Kituo hicho hiyo kufanya vizuri kitaaluma.
Amesema Shule hiyo kwa sasa inaendelea na mkakati wa kujenga madarasa mengine kwa ajili ya kuwapokea watoto wengi zaidi Januari mwaka 2022.
Amesema kituo hicho kilianzishwa Julai 20,2018 kikiwa na wanafunzi wawili wa kike na kiume na mwalimu mmoja ambapo hadi kufika sasa Desemba 2021 kituo kina watoto 36.
Naye Mathayo Mlegaiza akitoa salamu kwa niaba ya wazazi wanaosomesha watoto kituoni hapo, alipongeza uongozi wa kituo kwa kuwalea watoto wao kimaadili pamoja na kuwapatia taaluma, na kuahidi kwenda kuyaendeleza yale ambayo wamefundishwa shuleni hapo.
Mwalimu mkuu wa kituo hicho Rehema Saidi Mwendo amewashukuru wazazi kwa kuwaamini shule hiyo na kupeleka watoto wao na kulipa ada huku akiwahimiza wazazi kulipa ada kwa wakati.
Aidha amesema shule ipo kwenye mazingira bora na watoto hao waliohitimu elimu ya awali wamewafundisha vizuri na wanazungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...