Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya Biblia Takatifu kutoka kwa Askofu Mkuu wa kanisa la Wabaptist Tanzania Anorld Manase Molel, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. Desemba 21,2021.




MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip
Mpango leo tarehe 21 desemba 2021 amekutana na kufanya
mazungumzo na viongozi wakuu wa kanisa la Wabaptist Tanzania
wakiongozwa na Askofu Mkuu Anorld Manase Molel, mazungumzo
yaliofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais amewashukuru viongozi
pamoja na waumini wote wa kanisa hilo kwa kuendelea kuliombea taifa
katika kudumisha amani, umoja na mshikamano. Amesema jamii yeyote
yenye maadili mema na uzalendo inatokana na mchango mkubwa
unaotolewa na viongozi wa dini hapa nchini.

Amesema kanisa la Baptist limekuwa na mchango mkubwa katika
kushirikiana na serikali kutoa huduma za kijamii ikiwemo elimu na afya
hivyo amewaasa viongozi hao kuendelea kutoa huduma hizo ikiwemo
kufungua upya chuo kikuu walichokuwa wanakimiliki hapo awali cha
Mount Meru.

Amewasihi viongozi hao wa dini kuendelea kuwaombea viongozi wa
serikali ili kutenda yale yalio mema na kumtanguliza Mungu katika
utumishi wao. Amesema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi
viongozi wa dini wanapaswa kuwaelimisha wananchi kutumia mvua
zinazopatikana kufanya kilimo cha muda mfupi ili kujipatia mazao ya
chakula na biashara.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Anorld Manase
ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa uhuru wa kuabudu kwa
makanisa yote hapa nchini na kuahidi kanisa la Wabaptist Tanzania
litaendelea kuliombea taifa ili kuwepo Amani na mshikamano. Ameiomba
serikali kusimamia kikamilifu misamaha ya kodi inayotolewa kwa
makanisa wakati wa kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za elimu na
Afya.

Viongozi hao wa kanisa la Wabaptist Tanzania wameiomba serikali
kupitia upya sheria za usajili wa jumuiya za kidini hapa nchini ili kulinda
misingi iliowekwa kutoharibiwa kutokana na kuongezeka kwa huduma
hizo hapa nchini.

Aidha wamesema katika kuliletea taifa maendeleo wanaunga mkono
suala la sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022

na kuiomba serikali kuongeza kasi katika utoaji elimu ya sensa hiyo ili
wananchi wote watambue umuhimu wake
.
Katika hatua nyingine viongozi hao wa dini wameiomba serikali kuweka
mkazo katika masomo yanayowafanya wahitimu kujitegemea ikiwemo
masomo ya kilimo na biashara ili kuwawezesha kutotegemea kuajiriwa
pindi wanapohitimu masomo yao.

Makamu wa Rais amewahakikishia viongozi hao wa dini kwamba serikali
itaendelea kupokea ushauri na maoni kutoka katika taasisi za dini na
kuahidi changamoto zote walizozitoa kanisa la Wabaptist Tanzania
serikali ya awamu ya sita itazifanyia kazi.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi wakuu wa kanisa la Wabaptist Tanzania wakiongozwa na Askofu Mkuu Anorld Manase Molel, mazungumzo yaliofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. Desemba 21,2021.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa kanisa la Wabaptist Tanzania wakiongozwa na Askofu Mkuu Anorld Manase Molel (wa pili kutoka kulia kwa Makamu wa Rais ) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. Desemba 21,2021.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...