Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta (BLM) la Afya wa Jumuiya ya Afrika Masharikikatika ngazi ya Makatibu Wakuu unafanyika leotarehe 9 Desemba 2021katika Hotel Verde mjini Zanzibar.
Mkutano huu na mkutano wa ngazi ya MaafisaWaandamizi ambao ulifanyika tarehe 6 hadi 8 Desemba 2021 ni sehemu ya mikutano ya awali yenge jukukumu la kupitia na kuwasilisha agendana mapendekezo ya masuala ya afya ya kikandayatakayowasilishwa katika Mkutano wa 21 waBaraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiyaya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 10 Desemba 2021.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Dkt. Fatma H. Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Dkt. Othman Mohamed Ahmed, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Tanzania Bara, Bw. Eliabi Chodota, Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Dkt. Abdul S. Ali, Mganga Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkutano huu unafanyika mjini Zanzibar kwa lengo la kuendeleza jitihada za jumuiya katika kutangaza maeneo ya utalii ndani ya jumuiya. Vilevile kuvutia wageni na kuhamasisha utalii wa ndani kama ilivyosisitizwa katika maonesho ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-Tourism Expo) yaliyofanyika mapema mwezi Oktoba 2021 Jijini Arusha.
==============================
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Fatma H. Mrisho (Kulia) akifuatilia Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika leo tarehe 9 Desemba katika Hotel Verde mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota.
Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu, kutoka Kenya, Dkt. Moses Mbaruku (kati) akiongoza mkutano huo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Mhe. Chrisophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi kutoka Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kenya, Dkt. Kuria Francis.
Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Tanzania
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe kutoka Kenya
Ujumbe kutoka Uganda
Ujumbe kutoka Burundi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...