Na Said Mwishehe,Michuzi TV

VINARA wa kupinga ukatili wa kijinsia nchini Tanzania wametambuliwa na Umoja wa Ulaya kwa kupewa tuzo kama  ishara ya kuthamani kazi wanayoifanya huku ikielezwa kuwa mapambano  dhidi ya vita wa ukatikli wa kijinsia ni ya kila mmoja wetu.

Tuzo hizo zimetolewa jjini Dar es Salaam na kushuhudia na wadau kutoka mashirika,sekta binafsi,wadau wa kupinga ukatili pamoja na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambazo zipo kwenye umoja huo.

Akizungumza wakati wa tukio hilo la utoaji tuzo, Balozi wa Umoja wa Ulaya Fant amesema kuwa Dunia ipo katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na hivyo mataifa yote yanapaswa kuungana katika mapambano haya.

“Mapambano haya sio Tanzania pekee ila ni ulimwengu mzima, wote hivyo ni lazima tuungane kwa pamoja kuhakikisha ukatili wa kijinsia unapungua kwa kiasi kikubwa” Amesema Balozi Fanti.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni Ubalozi wa Ufansa Cecile Frobert amezungumzia Tamasha la hisani la kupinga ukatili wa Kijinsia lililoambatana na utoaji wa Tuzo mbalimbali kwa watu binafsi na Taasisi zilizoshiriki katika kutoa mchango wao kukomesha vitendo vya  ukatili wa Kijinsia hapa nchini ambapo wasanii walioshiriki Tamasha hilo waliimba nyimbo za jamii kupinga ukatili wa kijinsia.

Vinara hao licha ya kupatiwa Tuzo hizo pia walipata fursa ya kuzungumzia kazi zao wanazozifanya zilizowapelekea kufikia hatua hiyo.

Joyce Kiyango ni miongoni mwa watu waliopata Tuzo hizo ambapo amesema kuwa hilo limetokana na ubunifu alioufanya kufundishia wanafunzi wake nakwamba ubunifu huo umemuwezesha kuzaa matunda kutokana na watoto wake kupenda masomo darasni na kuondoa kabisa tatizo la utoro.

“Nimejisikia furaha sana kupata Tuzo hii mana hiki ni kitu ambacho nilikua nafanya tu ili watoto wapende masomo lakini sikutegemea kama ingenifanya kufahamika na kufikia hapa leo, kwakweli imenipa faraja sana” alisema Joyce.

Aidha Balozi Fanti alipata fursa ya kukabidhi Tuzo kwa moja ya mshindi wa Tuzo hizo Pili Maguzo Mkurugenzi wa Bahati Fimale Band kutokana na kazi wanazofanya katika kutunga na kuimba nyimbo za kuielimisha jamii na kupinga.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fanti (kulia) akikabidhi Tuzo kwa kwa Pili Maguzo (kushoto) Mkurugenzi wa Bahati Fimale Band kutokana na kazi wanazofanya katika kutunga na kuimba nyimbo za kuielimisha jamii na kupinga ukatili wa Kijinsia.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fanti akizungumza kwenye Tamasha la hisani muda mfupi kabla ya kukabidhi Tuzo.
Mwalimu Joyce Kiyango (kushoto) wa Shule ya Awali ya One Planet iliyopo Dodoma akipokea Tuzo yake aliyoipata kutokana na umahiri wake wa kuwafundisha watoto kwa namna ya kucheza nao muziki na michezo mbalimbali.
Balozi wa Ujerumani nchini Regine Hess akizungumza wakati wa Tamasha hilo kabla ya kukabidhi Tuzo.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni Ubalozi wa Ufansa Cecile Frobert akizungumza kwenye tamasha hilo.

Wasanii kutoka katika Bendi za Muziki wa Kitanzania wakitumbuiza kwenye tamasha hilo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...