Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Imeelezwa kuwa malezi na makuzi mema kwa Watoto ni msingi thabiti wa kuandaa familia bora na Taifa lenye viongozi waadilifu.
Kwa
nyakati tofauti baadhi ya Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wamesema kuwa
Wazazi kutotimiza wajibu wao wa malezi na makuzi bora kwa watoto
imekuwa ikichangia kuwa na viongozi wasiokuwa waadilifu tangu ngazi ya
familia,hadi Taifa.
Wameeleza
kuwa Vijana wanaotumia Dawa za kulevya,pamoja na Viongozi wapenda
rushwa, wabadhirifu wa fedha,na rasilimali za Taifa ni matokeo ya Wazazi
na Walezi kushindwa kutimiza wajibu wao wa malezi na makuzi mema kwa
Watoto wao.
Wananchi hao
wameshauri Wazazi na Walezi kuwekeza kwenye malezi na makuzi mema ya
Watoto ili kuandaa familia Bora na viongozi waadilifu katika Taifa la
Tanzania.
Wamesema
familia zina wajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika
misingi imara ya dini zao ili waweze kuwa na hofu ya Mungu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...