Na John Mapepele.
Mashindano ya Taifa CUP 2021 kesho Disemba 14, 2021 yanaingia kwenye nusu fainali kwa soka ya wanaume, wanawake na netiboli huku michezo ya riadhaa na maonesho ya Sanaa yanatarajiwa kuanza kwa kishindo kikubwa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa (BMT) ambaye ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya Taifa CUP 2021 amesema mashindano yanaendelea vizuri tayari timu zimeshafuzu kucheza nusu fainali za mashindano hayo hapo kesho.
Ametaja timu za mikoa zilizoingia nusu fainali soka upande wa wanaume kuwa ni Mjini Magharibi itakayocheza na Ruvuma saa moja katika uwanja wa uhuru na Mara itakayocheza na Dodoma katika uwanja huohuo majira ya saa kumi jioni.
Kwa upande wanawake timu zilizofuzu nusu fainali za mashindano hayo ni mkoa wa Dar es Salaam utyakaocheza na Kusini Unguja uwanja wa uhuru majira ya saa tatu na Mkoa wa mara utakaocheza na Arusha saa nane mchana kwenye uwanja huohuo.
Aidha, Bi Msitha asema timu zilizoingia nusu fainali kwa upande wa Netiboli ni Pwani itakayocheza na Mjini Magharibi uwanja wa Benjamini Mkapa saa mbili na timu ya Dodoma itakayovaana na Dar es Salaam majira ya saa nne katika uwanja huo huo.
Wakati huo huo kesho ni uzinduzi rasmi wa riadha kwa mbio fupi na ndefu ambapo pia kuanzia saa moja usiku kutakuwa na mashindano ya sanaa za maonesho ya fani ya muziki wa Singeli na kizazi kipya.
Amesema kamati imeandaa watalaam wa muziki na wasanii wakongwe ambao watakuwa na program kabambe ya kuwanoa washiriki ili waweze kuonyesha vipaji vyao.
Mchezo wa soka kwa wanawake baina ya timu ya Iringa na Mjini Magharibi leo Disemba 13,2021 jijini Dar es Salaam ambapo Mjini Magharibi ilishinda kwa Penati (7-6) katika mashindano ya Taifa CUP 2021.
Mchezo wa soka kwa wanaume baina ya timu ya Pwani na Dodoma leo Disemba 13,2021 jijini Dar es Salaam ambapo Dodoma ilishinda 3-2 katika mashindano ya Taifa CUP 2021.
Kikao cha pamoja kilichowajumuisha wataalam wa Muziki, Wasanii na Kamati ya Taifa CUP 2021 wakijadili maandalizi ya mashindano sanaa za maonesho ya fani ya muziki wa Singeli na Kizazi kipya yatakayoanza kesho Disemba 14,2021 uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...