JESHI a Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Mzee mwenye umri wa miaka 61 kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne 

Akizungumza leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga amesema mzee huyo  kwa sasa anashikiliwa na jeshi hilo ili sheria ichukue mkondo wake.

Katika tukio lingine Kamanda Lyanga amesema
Katika Wilaya ya Kongwa, Polisi wanamshikilia mwanaume wa miaka 30 kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 75, tukio lililotokea wilayani Kondoa.

Mbali na tukio hilo jeshi hilo limemkamata mwanaume (30) kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kiume katika mtaa wa Mulua wilaya ya Kondoa

Aidha, Jeshi hilo linamshikilia mwanamke (24) mkazi wa Tampoli wilaya ya Kondoa kwa kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi ambapo amemchoma kwa kitu cha ncha kali tumboni mume wake baada ya kumkuta amesimama na mwanamke mwingine,na majeruhi amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kondoa

“Watuumiwa hawa wote tumeshawakamata na jitihada za kuwafikisha katika mikono ya sharia ili wakakumbane na huo mkono zinaendelea,”amesema Kamanda Lyanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...