*Yawataka kuwa wabunifu na wenye weledi

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imekitoza faini ya shilingi milioni mbili kituo cha utangazaji cha wasafi Tv kwa kosa la kurusha kipindi kisicho na maadhui kwa jamii kupitia chaneli yake ya 'youtube' katika kipindi  kinachorushwa siku ya Jumapili.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam mwenyekiti wa kamati ya maudhui mamlaka ya mawasiliano TCRA Hansi Gunze amesema Novemba 1, 2021 mtangazaji wao Jordani Mwasha katika channeli ya youtube alifanya mahojiano na nabii Shilaa ambaye alitoa kauli chafu kukejeli dini ya kikristo kwa kumuita Yesu tapeli alikua anapenda matajiri ambapo kitendo hicho ni uvunjaji wa kanuni za maaudhui

Hata hivyo amesema kutokana na kitendo hicho cha kukashifu dini ya kikristo kituo hicho walishusha video zote na kuomba radhi kupitia kurasa zake za mtandaoni kwa watazamaji wake hivyo pamoja na kukiri na kuomba radhi TCRA wamewapa onyo kali na kuwataka kuendelea kuomba radhi kwa jamii kupitia channeli zao zote kwa kurusha tangazo litakalopigwa mara tatu kwa siku kuanzia saa nne asubuhi siku tatu mfululizo

Sanjari na hayo amekitaka chombo hicho kinahakikisha shughuli zake za kuhabarisha Umma wanazingatia kanuni na sheria zilizowekwa pamoja kuajiri wafanyakazi walio na weledi na wahariri mahiri ambao kabla ya habari kurushwa wanaipitia vizuri ili kuondoa ukakasi kwa jamii na sintofahamu kwa watazamaji.

"Niwaase kuhakikisha vipindi vya dini vyote viwe na wahariri mahiri wenye utaalamu waadilifu kwani kufanya hivyo kutawasadia kuepuka adhabu zisizo na tija"alisema Gunze

Kwa upande wake mkurugenzi wa vipindi kituo cha wasafi Spensa Lameki ameishukuru Mamlaka hiyo na amekiri kutoruhusu kosa kama hilo kujirudia tena na adhabu walizopewa watazitimiza .
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Hans Gunze akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa hukumu ya dhidi Wasafi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiluano Tanzania (TCRA) Hans Gunze akimkabidhi Hukumu Mkurugenzi wa Habari wa Wasafi Spencer Lamack baada ya kusomewa hukumu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA wakiwa katika hukumu ya wasafi.

Mkurugenzi wa habari wa Wasafi Media Spencer Lameck akizungumza kuhusiana na hukumu hiyo na kudai watafanyia kazi yale yaliyomo kwenye hukumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...