Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Kutoka katika mradi wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambamo dhidi ya UVIKO-19 Halmashauri ya Manispaa ya Singida imepokea shilingi Milioni 740 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 37 katika shule za Sekondari Wilayani humo.

Akiwa ziarani Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amekagua ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa katika shule ya Sekondari Mandewa kwa niaba ya vyumba vyote 37 vilivyojengwa katika Manispaa ya Singida.

Akiwa shuleni hapo Waziri Ummy ameridhishwa na ujenzi wa madarasa hayo na amepongeza Uongozi wa Manispaa ya Singida kwa usimamizi makini wa ujenzi wa madarasa hayo.

Pia amesema Serikali italeta fedha za kukamilisha bweni lililoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi katika Sekondari hiyo iliwezekana kuanzia mwaka 2022 Shule hiyo ipewe kibali cha kupokea wanafunzi wa kidato cha Tano na sita kwa mchepuo wa Sayansi.

Nimmepata taarifa kuwa hakuja shule ya A’ level ya Wasichana ya Sayansi kwa hiyo tutaleta fedha za kukamilisha bweni ili shule hii iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano ili watoto wa Singida wanaofauli kidato cha nne wapate fursa ya kuchaguliwa hapa karibu’

Naye Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe amesema wanafunzi wanaotegemewa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2022 ni 3,976 na waliomaliza kidato cha nne ni 1,921 hivyo kuna ongezeko la wanafunzi takribani 2000 bila kupata madarasa haya hali ingekua mbaya lakini sasa hakuna changamoto yeyote na wanafunzi wote wataanza masomo ya awamu moja.

Shule ya Sekondari Mandewa ina jumla ya wanafunzi 1,282 na ilipokea fedha shilingi milioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 6 ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...