Kijana EZRA MWAIKAMBO mkazi wa Kiwalani Dar es salaam ameibuka mshindi baada ya kujinyakulia pikipiki aina ya Boxer kupitia KAMPENI YA TIGO "WAGIFTISHE GIFT JUU YA GIFT".
Ikiwa ni wiki ya pili tangu kuanza kwa kampeni hiyo inayoendeshwa kidijitali, Tigo Tanzania.
Akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa pikipiki mshindi huyo ameishukuru Tigo kwa kuwajali wateja wake huku akieleza matarajio yake kuwa ataenda kuanzisha biashara ya usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda na hivyo kumuwezesha kujiajiri yeye mwenyewe na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Akimpongeza mshindi wa pikipiki hiyo pamoja na washindi waliojishindia simu janja Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini ROBERT KASUGA amesema katika mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidijitali nchini, kampuni ya Tigo imewahakikishia wateja wake kuwa kila mtu anapata nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu zaidi kwa kila ununuzi wa simu za kisasa za ITEL T20 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote, hivyo akawaomba wateja waendelee kununua simu za ITEL T20 kutoka maduka ya Tigo nchini kote ili kuingia kwenye droo ya kupata nafasi ya kujishindia moja ya pikipiki kati ya 5 zikiwemo simu janja zinawaniwa katika promosheni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...