Mwezeshaji wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kivule Zahara Mzee akiwasilisha mada katika semina hiyo iliyokutanisha mtandao wote wa vituo hivyo na kwa pamoja wamedhamiria kuendeleza vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa jinsia hasa kwa wanawake na mabinti.
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP,) umekutana na wadau wa vituo vya Taarifa na Maarifa kwa Kata 18 za jiji la Dar es Salaam na kutafakari mikakati ya mwaka 2022 katika harakati za kupinga ukatili wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Akizungumza katika semina hiyo ya mwisho ya mwaka 2021 mwezeshaji kituo cha Taarifa na Maarifa Kivule Zahara Mzee amesema kuwa mikakati iliyojadiliwa na vituo hivyo kutoka Kata 18 za Mkoa wa Dar es Salaam ni pamoja na tafakari ya mwaka 2021, vipaumbele vya mwaka 2022 pamoja na ratiba ya mwaka ya GDSS.
Amesema mapendekezo yaliyofikiwa na wanadau wa mtandao wa vituo hivyo vya Taarifa na Maarifa ni pamoja na kila mmoja awe mwanachama wa vituo vya Taarifa na Maarifa, kutolewa kwa elimu ya uundaji wa vituo vya Taarifa na Maarifa, kupewa elimu juu ya kuandika taarifa na ripoti, kupewa nyaraka muhimu kwa utendaji pamoja na kutunza taarifa za matukio kwa mwaka mzima.
Aidha amesema kuwa, wanamtandao wa vituo hivyo Kwa mwaka ujao wameomba kukutana naviongozi wa vituo na Mkurugenzi mtendaji wa TGNP ili kushirikishana mafanikio na changamoto za vituo hivyo pamoja na kupewa vyeti vya utambuzi kwa wadau hao.
''Tumekuwa tukikabiliana na changamoto na mafanikio katika uendeshaji wa vituo hivi tunaomba kukutana na viongozi akiwemo Mkurugenzi wa TGNP na kujadili changamoto ili tuweze kuyafikia malengo ya kutokomeza vitendo vya ukatili na kuwainua wanawake.....Tunapendekeza kuendeleza matamasha zaidi pamoja na kuwatambua wana GDSS kwa kutoa vyeti ya utambuzi ili kuleta ari zaidi katika jamii.'' Amesema.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa kituo cha Taarifa na Maarifa Ubungo Bi. Neema Mwinyi amesema mwaka 2021 umekuwa bora hasa kwa kushirikiana na Serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kushirikisha kwa ukaribu na vituo hivyo katika ngazi ya maamuzi katika masuala mbalimbali ya kijamii hasa katika masuala ya ukatili yanayotokea katika ngazi za mitaa na kata.
Ameeleza kuwa kupitia vituo hivyo vya Taarifa na Maarifa wamesambaa katika Kata 18 jijini Dar es Salaam na mikakati ya pamoja inayotengenezwa ni ya kushirikishana ili kuweza kupata ufumbuzi na kwa mwaka ujao wana GDSS watakuwa sehemu ya kutoa mada kwa kila Kata na kuonesha yale wanayoyafanya
Amesema TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na vituo hivyo na kuiomba kuzidi kuwainua kwa kutoa mafunzo zaidi katika kujenga jamii imara yenye usawa.
Kata zilizoshiriki mkutano huo ni pamoja na Saranga, Kivule, Kipunguni, Mabibo, Makumbusho, Makumla, Zingiziwa, Ubungo, kimara, Saranga, Manzese,Temeke, Kisarawe, kitunda, Chanika.
wadau wakichangia mada.
Mwezeshaji wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kivule Zahara Mzee akiwasilishamada katika semina hiyo iliyokutanisha mtandao wote wa vituo hivyo na kwa pamoja wamedhamiria kuendeleza vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa jinsia hasa kwa wanawake na mabinti.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...