Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu amesema
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wanapaswa kuendana na mabadiliko ya
Teknolojia wakati akifungua Mkutano
Mkuu wa Mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu unaofanyika kwa
siku tatu kuanzia leo Desemba 01 hadi Desemba 03 mwaka 2021.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Dkt. Kazungu amesema
Wahasibu na Wakaguzi wa fedha ni watu muhimu katika maendeleo hususani
uchumi wa viwanda hivyo wanapaswa kujipima na kuona umuhimu wao katika
jamii.
"Wahasibu
ndiyo wanaofanya uchambuzi wa mambo ya fedha na kuandaa ripoti za
hesabu za fedha na uhakika ambazo zinasaidia katika ukusanyaji wa kodi,
kuimarisha uchumi na kuvutia uwekezaji," Amesema Kazungu.
Amesema
katika wimbi hili la Mapinduzi ya Viwanda ambayo yanahusisha teknolojia
hivyo wanapaswa wajipange vizuri Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ili
kuendana na mapinduzi hayo, pia amesema suala la maadili ni suala nyeti
kwenye utumishi wa umma hususani kwanye taaluma ya Uhasibu kwasababu
Wahasibu ndio wanaotunza hesabu hivyo inabidi wasimamie maadili ili
kuepuka hati chafu kwenye Taasisi mbalimbali.
Pia
amesema Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wanayo nafasi kubwa kufanikisha
safari ya uchumi wa viwanda, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa
kujiona kuwa ana deni kwa Taifa ili kufikia malengo yaliyowekwa na
Serikali.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu amesema
katika mageuzi ya teknolojia na mapinduzi ya kiuchumi duniani
inahitaji Wahasibu ambao wanaweza kwenda na teknolojia pamoja na kuwa
uwezo wa kuchakata takwimu mbalimbali ambazo zinaongeza tija na thamani
katika maeneo mbalimbali ya kazi.
Amesisitiza
kuwa elimu waliyonayo Wahasibu haitoshi kwa sasa hivyo wanapaswa
kuelewa vizuri mabadiliko ya Teknolojia hasa kwenye ukuaji wa uchumi wa
Taifa bado wanahitajika Wahasibu wengi kwani wahasibu waliopo hawatoshi
hivyo zitolewe elimu kwenye vyuo pamoja na shule ili kuleta hamasa kwa
wanafunzi kupenda fani hiyo.
Pia
amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa mwenyekiti wa wa
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwani
nafasi hiyo ni nzito hivyo atasimama vizuri ili kuweza kufikia malengo
waliyojiwekea kama Bodi.
Akizugumza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema
kwamba Bodi hiyo ina majukumu makubwa matano ambayo ni kusajili
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu. Kusimamia taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi,
kusimamia mafunzo na kutoa vyeti vya kitaaluma, kutoa muongo wa
utayarishaji wa hesabu na ukaguzi wa hesabu.
Amesema Bodi
hiyo inazingatia viwango vya kimataifa vya uandishi wa vitabu na
ukaguzi. Hivyo Tanzania kupitia NBAA inaendelea kusimamia matumizi ya
viwango vya kimataifa vya utayarishaji na ukaguzi wa taarifa za fedha
katika Serikali Kuu na idara zake, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya
kiserikali (NGOs) kwa kushirikiana na Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wa
hapa nchini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu
akizungumza kuhusu Serikali inavyothamini mchango wa Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu hivyo itasimamia taaluma hiyo wakati wa ufunguzi wa
mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu
ulioandaliwa na Bodi ya NBAA uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika
hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu
alimwakilisha Waziri Wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa
Sylvia Temu akizungumza kuhusu namna alivyojipanga kama Mwenyekiti mpya
pamoja na kusimamia ipasavyo Bodi hiyo ili kuweza kufikia malengo
waliyojiwekea ili kuendana na Kauli ya Rais Samia ya Kazi iendelee
wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi
wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC
Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania
(NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza kuhusu namna Bodi hiyo
inavyofanya kazi pamoja na mafanikio waliyoyapata ndani ya muda mchache
wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi
wa Hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC
Bunju jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa, wanyakazi wa Bodi ya NBAA, Wahasibu na Wakaguzi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu aliyemwakilisha
Waziri Wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika
ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Wahasibu na Wakaguzi uliofanyika leo Desemba
01, 2021 katika Hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo akitoa neno la shukrani
kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt.
Khatib Kazungu aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango ufunguzi wa
mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu
ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)
uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu akiwa
kwenye picha ya pamoja na Wadhamini, Viongozi mbalimbali wa Serikali na
Bodi hiyo pamoja na Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu wakati wa ufunguzi
wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu
ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...