MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ngorongoro kupitia chama cha ACT wazalendo Johnson Mahuma amesema endapo wananchi wa jimbo hilo watampa ridhaa ya kuliongoza Jimbo Hilo atapeleka kilio cha changamoto ya barabara inayotoka mto wa mbu kuelekea Loliondo ambayo ndio kilio kikubwa kwa wananchi wa Tarafa ya Loliondo
Akizindua Kampeni za kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya ubunge kwa jimbo la ngorongoro mgombea ubunge kwa chama cha ACT Wazalendo Johnson Mahuma anasema kilio kikubwa kwa wakazi wa jimbo hilo ni Barabara inayotoka mto wa mbu kuelekea Loliondo na endapo atapata ridhaa atapeleka changamoto hiyo bungeni
Mahuma amesema kilio Cha wananchi kutokana na ubovu wa barabara hiyo kina zaidi ya miaka 60 Hali inayosababisha wakazi wa Loliondo kufata bidhaa nchi jirani ya Kenya hivyo kujengwa kwa barabara hiyo kutawafanya wananchi kupata bidhaa za kiurahisi tofauti na ilivyo Sasa.
"Ukiangalia kwa Sasa kuliko mwananchi wa hapa akachukue bidhaa Arusha Yuko radhi aende nchi jirani ya Kenya, Sasa mkinichagua nitapambana na hii changamoto"Alifafanua.
Aidha Mahuma Alifafanua kuwa Ngorongoro ni miongoni mwa majimbo yanayokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo,migogoro ya Mara kwa Mara,maji,pamoja na mazingira magumu ya watoto kupata elimu
Awali wananchi wa Tarafa ya Loliondo wakimuuliza maswali mgombea huyo walitaka kujua endapo mgombea atawezaje kuzitatua changamoto nyingi zinazolikabili jimbo hilo ikiwemo migogoro ya mara kwa mara ambayo watangulizi walishindwa kuitatua
"Hebu tuambie wewe utawezaje Kutatua migogoro inayotukabili au ndo unataka kura tukishakuchagua utuache uende mjini"?Aliuliza Saruni Losioky mkazi wa Loliondo.
Akijibu changamoto hizo Mgombea huyo akawataka wananchi kumpa uwakilishi ili kufikisha kilio chao bungeni na kwamba changamoto hizo zitatatuliwa endapo wananchi watakubali kufanya mabadiliko
"Tusiishi kwa kukariri Mimi sitakuwa Kama viongozi waliopita nijaribuni kwa kunipa kura muone nitakatoyafanya"Aliongeza Mahuma.
Jimbo la ngorongoro linafanya uchaguzi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Willium Tate Olenasha mbapo mpaka sasa tayari vyama sita tayari vimekwishachukua form za kuomba ridhaa ya uwakilishi katika Jimbo Hilo.
Miongoni mwa vyama ambavyo mpaka Sasa vimekwishazindua kampeni ni pamoja na CCM,ACT Wazalendo, NLD,UDP,SAU, na NRA tayari kwa maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Dec.11 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...