*Ni Wateja 5000 kunufaika na mafuta ya bure 

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV.
SHIRIKA la Bima la Taifa ((NIC) lamwaga mafuta kwa wateja wenye  bima ya shirika hilo  ikiwa ni kurudisha  upendo kww wateja na kuthamini mchango wao wa kuchangua NIC.

NIC imekuja na romosheni ya kutoa mafuta kwa wateja ambayo inakwenda kwa  JIKAVE NA NIC ambapo kupitia promosheni hiyo wateja 5,000 watakaokata Bima kubwa magari yao yatajaziwa mafuta kuanzia lita tano hadi lita 100 kutegemeana na kiasi cha  Bima watakacholipa.

Akizungumza kwenye uzinduzi promosheni hiyo  leo Jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Elirehema Doriye amesema promosheni hiyo itaisha mara tu magari 5,000 yatakapofikiwa hivyo basi amewataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo ya kukata bima ya NIC.

"Promosheni hii ni ya nchi nzima Bara na Visiwani na pale tu mteja atakapokata Bima kubwa atapokea ujumbe papo hapo utakaomjulisha namna ya kujipatia zawadi yake katika mkoa wake alipo na kupata mafuta katika kituo cha mafuta PUMA". Amesema 

Amesema amewasihi watanzania kuchangamkia bidhaa za Bima nyingine ambazo NIC wanatoa kwa wateja wao ili waweze kufaidika na promosheni nyingi zinazoolewa na Shirika hilo na hakuna shirika la bima  ambalo linaweza kutoa mafuta bali ni NIC pekee kwa kuwa Sisi Ndiyo Bima.

Kwa upande wa Mteja wa NIC   Ben  Mwaipaja ameushukuru uongozi wa NIC kwa utaratibu ambao wameufanya hivyo ameridhika na huduma zinazotolewa na Shirika hilo na kuamua kukata Bima ya Gari yake kupitia NIC.

"Nawashauri wateja wengine wenye vyombo vyao vya moto, wenye nyumba zao wanaotaka kukatia Bima basi waje NIC ambayo imeboreshwa na inamabadiliko makubwa sana na ninashukuru kwa utaratibu huu na nimepata mafuta yangu asanteni sana". Amesema Bw.Mwaipaja

Nae Kiongozi wa Madereva Bodaboda Fire Kariakoo Bw.Jaffari Hassan ameishukuru NIC kwa promosheni hiyo kwani wao wamekata Bima mwezi uliopita na sasa promosheni hiyo imewangukiwa wao na kuweza kujaziwa mafuta kwenye pikipiki zao hivyo wataendelea kuwahimiza madereva wengine wa bodaboda waweze kukata Bima kupitia Shirika la Bima la Taifa NIC.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Promosheni ya JIKAVE Na NIC ya kutoa mafuta kwa wateja wake wenye bima ya NIC katika Kituo cha Mafuta cha PUMA Fire Kariakoo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akijaza mafuta kwa Mteja wa NIC Ben Mwaipaja  (katikati) na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yessaya Mwakifulefule (watatu kutoka kulia) ujazaji wa mafuta kwa wateja wa umefanyika katika Kituo cha Mafuta cha Puma Fire jijini Dar es Salaam.Mteja wa NIC  Ben Mwaipaja  akizungumza na waandishi  wa habari mara baada ya kujaziwa mafuta na NIC katika kituo cha mafuta cha Fire Kariakoo jijini Dar es Salaam.Kiongozi wa Bodaboda Fire Jaffar Hasaan akizungumza na waandishi  wa habari mara baada ya kujaziwa mafuta na NIC katika kituo cha mafuta cha Fire Kariakoo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akijaza mafuta kwa Mteja wao Bodaboda, ujazaji wa mafuta kwa wateja wa umefanyika katika Kituo cha Mafuta cha Puma Fire jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...