BENKI ya NMB imeahidi kushirikiana na Taasisi ya Mbeya Family Group (MFG,) katika jitihada zao za kuinua jamii kupitia shughuli wanazozifanya ambazo pia zina kipaumbele na benki hiyo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya shule, hospitali na kuinua jamii kwa ujumla.
Akizungumza katika mkutano mkuu uliokwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi wa taasisi hiyo Mkuu wa Idara ya Bima kutoka NMB Martin Massawe ambaye alimwakilisha Afisa Mtendaji mkuu wa benki hiyo Bi. Ruth Zaipuna amesema, umoja huo ni wa mfano kwa kuwa umekuwa ukisaidia jamii bila kujali itikadi ya aina yoyote ile.
''Nipo katika idara ambayo inawahusu mkiwa kama kikundi, suala la bima ya afya ni muhimu kwa kila mmoja kwa sasa, naahidi tutakutana na viongozi wenu na kupitia taarifa zenu mlizosajili na tutalishughulikia hilo kwa mafanikio makubwa...NMB inafanya kazi kwa ukaribu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF,) kupitia 'NMB Dunduliza' naamini tutafanikisha hili na kila mmoja wetu atapata bima ya afya.'' Amesema.
Kuhusiana na suala la kuanzishwa kwa SACCOS kwa kikundi hicho Massawe amesema kuwa watashughulikia suala hilo kwa ukaribu na uongozi, pamoja na kushiriki nao katika uboreshaji wa miundombini mashuleni kupitia 'NMB Foundation maalum kwa kurudisha jamii ambapo hadi sasa shilingi bilioni 10 zimetumika katika kufanya maboresho mashuleni kwa miezi sita pekee.
''Leteni mapendekezo juu ya mpango wa kuanzisha SACCOS ninatumaini tutafika sehemu nzuri...kuhusiana na suala la ufadhili wa mikutano ya namna hii naomba tupewe taarifa mapema ili tuweze kushiriki kwa namna yoyote.'' Amesema.
Pia amewashauri kutumia umoja huo kutafuta fursa za kiuchumi na kushirikiana bila ubinafsi na mafarakano ili waweze kuwafikia wanajamii wengi zaidi katika maeneo mbalimbali nchini.
Awali Mwenyekiti wa taasisi hiyo Michael Mwangoka alieleza kuwa kikundi hicho kinahusisha wazaliwa, wakazi, waliosoma, na waliowahi kuishi jijini Mbeya bila kujali itikadi za dini, siasa na ukabila na hadi sasa kuna washiriki wapatao 150.
''Lengo la umoja huu ni kufarijiana na kusaidia wakati wa shida na raha pamoja na kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa majengo katika shule ya Majengo, Mbeya ambapo tulifanya ukarabati uliogharimu shilingi ilioni 20 zilizochangwa na wanachama...Ninaamini NMB mkitufadhili katika SACCOS yetu tutafika mbali zaidi.'' Amesema.
Mwangoka amesema, tayari wamesajili bima ya mazishi kupitia benki ya NMB na kukua kwa kasi kwa taasisi hiyo wameona ni muhimu kuwa na SACCOS na tayari jambo hilo limekwishawasilishwa kwa wadau hao kwa utekelezaji zaidi.
Mkutano huo umehudhuriwa na wakazi wa Mbeya waishio katika Mkoa huo na kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam , Dodoma na waishio nchi za Malawi, Uingereza na Australia.
Mkuu wa Idara ya Bima kutoka Benki ya NMB Martin Massawe akizungumza katika mkutano huo na kueleza kuwa watashirikiana na taasisi hiyo katika mapendekezo waliyoyatoa na kuwashauri kuendeleza umoja huo bila mafarakano. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mbeya Family Group (MFG,) Michael Mwangoka akizungumza katika mkutano huo na kueleza kuwa taasisi hiyo inakuwa kwa kasi na tayari imeshiriki shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa, dini wala makabila. 
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Mbeya Family Group (MFG,) Juma Abinala akizungumza wakati wa mkutano na kueleza kuwa wamelenga kuwafikia wanajamii wengi zaidi.
Mwenyekiti wa Matukio wa MFG Rose Mkisi akizungumza katika mkutano huo ambapo amewashukuru wanachama wa Taasisi hiyo kutoka ndani na nje ya nchi kwa kuonesha ushiriki wao, Leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa MFG Bi. Asha Ibrahim akizungumza katika mkutano huo na kueleza kuwa wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali ya shida na raha. 
Matukio ya utoaji vyeti ya heshima na utambuzi kwa wadhamini na viongozi waliofanikisha kufanyika kwa mkutano huo.
Matukio katika picha.
Wanachama waTaasisi ya MFG wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Martin Massawe (Mwenye suti nyeusi,) ambaye ni Mkuu wa Idara ya bima kutoka benki ya NMB.
Matukio mbalimbali katika picha za Mkutano mkuu wa MFG uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...