Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha SP Solomoni Mwangamilo akisisitiza jambo kwa madereva katika Stendi kuu ya mabasi Mkoani Arusha Leo 18/12/2021
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha SP Solomoni Mwangamilo akiteta jambo na baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani mkoa wa ArushaNa. Vero Ignatus, Arusha
Katika Kuelekea Msimu wa sikukuu za Mwisho wa mwaka, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha usalama Barabarani kimefanya ukaguzi wa zaidi ya magari(100) na kutoa elimu kwa madereva na abiria wanaotumia vyombo vya moto kwenda mikoa mbalimbali hapa Nchini.
SP Solomoni Mwangamilo ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha ,amezungumza na madereva hao leo December 18.2021 katika stand Kuu ya mabasi,ambapo ametoa onyo kwa baadhi ya madereva wanaoendelea kuendesha magari ya hayo kwa mwendokasi .
Mwangamilo amesema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya madereva hao wanaokiuka Sheria na kanuni za Usalama barabarani, ambapo kumekuwepo na tabia ya baadhi ya mdereva kubashiri (BET) ili kuwahi kufika wanakokwenda, amewataka kuacha mara moja tabia hiyo.
Aidha, amewataka Abiria/ wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale wanapowaona madereva wanaokiuka sheria za usalama Barabarani na kwenda mwendokasi ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika
Vilevile Mwangamilo emeendelea kusisitiza madereva kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili kupunguza ajali hasa kipindi hiki ambacho kuna wingi wa magari barabarani ya Abiria pamoja na magari binafsi
Kwa upande wake Abiria Seleman Kalinde wamelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, hususani Kikosi cha usalama Barabarani kwa kuwa na utaratibu wa mara kwa mara kukagua vyombo vya moto, hasa kipindi hiki ambacho wamiliki wengi hutumia fursa ya sikukuu za mwisho wa Mwaka kurejesha magari yao Barabarani.
Husein Mfinaga ni mmoja Kati ya baadhi ya madereva, wamelishukuru Kikosi Cha usalama Barabarani kwa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa madereva na abiria, ili kuweka uelewa wa pamoja ili kuepusha ajali zisizo za lazima Barabarani.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...