Na Abdullatif Yunus - Michuzi Kagera.

Nguli wa Muziki wa Kizazi kipya na Kufoka foka maarufu kama Hip Hop, Msanii Joseph Haule (Profesa Jay) pamoja naye Nay wa Mitego ni miongoni mwa Wasanii wakubwa watakaongoza safu ya Burudani katika Tamasha la Mwisho wa Mwaka Mkoani Kagera.

Tamasha hilo lijulikanalo Kama Kagera Desemba Festival 2021 kinafanyika Desemba hii siku Mbili mfululizo Tarehe 25 na 26 Sikukuu ya Krismasi katika eneo la mapumziko ECO BEACH Hotel Iliyopo Bukoba Manispaa ambao ndio waandaji wa Tamasho hilo la Kiburudani.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa Eco Beach Ndg. Jackson amesema Maandalizi ya Tamasha hilo yanaendelea vizuri na kwamba kwa Upande wa Wasanii tayari PROFESA JAY na Nay wa Mitego wamethibitishwa kuwepo, huku Msanii mwingine anayefanya muziki wa karaoke Zarry Edosha kutoka Jijini Mwanza ataungana nao pia.

 "...Tunataka tuwafanyie Wana Kagera waishio hapa na wale wanaokuja likizo wapate Burudani Nzuri tofauti na kile walichokizoea, ndio maana tulianza mapema kujiandaa na Sasa tunakamilisha Baadhi ya Mambo, Jambo la Msingi wahudhulie kwa Wingi kwani Burudani Ni nyingi waje na familia zao, Watoto watapata nafasi ya kucheza Michezo yao,  Mashindano ya kuimba kucheza pool na mengine mengi.."* amesema Jack

Hata hivyo Tamasha hilo la Kagera Desemba 2021, linaonekana kuendelea kuteka hisia za wapenda Burudani kwa kuzingatia Ukubwa wa Tamasha lenyewe na Maandalizi, ambapo mbali na Kiingilio cha shilingi elfu Kumi kwa Nafasi za Kawaida, pia zipo Meza zinazoendelea kuuzwa Shilingi laki 2, laki 5 na Milioni Moja.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...