Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP Salum Hamduni amesema kuwa kwa kiwango kikubwa Rushwa imedhibitiwa nchini kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Idara, Taasisi mbalimbali na Wananchi katika kupambana nayo.

CP Salum Hamduni ameyasema hayo katika Siku ya Maadili na Haki za Binadamu iliyoadhimishwa leo, Desemba 10, 2021 Kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, ikihudhuriwa na Wananchi, Idara, Taasisi mbalimbali nchini.

CP Hamduni amesema suala la kupambana na Rushwa linahitaji jitihada, nguvu ya pamoja na ushirikiano ili kutokomeza kabisa, kuanzia kwa Watumishi wa Umma, Sekta Binafsi na hata mtu mmoja mmoja.

“Rushwa ndani ya nchi hii haina nafasi, na ili tutokomeze kabisa suala hili la Rushwa linahitaji ushirikiano wa hali ya juu, kuunga nguvu ya pamoja ili kupambana nayo ipasavyo na kuitokomeza kabisa katika nchi hii”, amesema CP Hamduni

“Ili kukabiliana nayo hatua ya kwanza, kuikataa, kuelimisha, kupambana nayo, kuchunguza na kukamata, na sisi tumejielekeza zaidi kutoa elimu, kuelimisha Umma, kufanya utafiti kuhakikisha Rushwa inadhibitiwa kabla haijaeleta madhara kwa nchi yetu”, ameeleza

Pia, amewaasa Wananchi kutoa taarifa za Rushwa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na TAKUKURU ili taarifa hizo zifanyiwe kazi ili kuitokombeza kabisa.

Kwa upande wake, Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi amesema kwa upande wa maadili kwa Watumishi wa Umma, ameeleza kuna wakati maadili yanaenda vizuri lakini kuna wakati maadili yanaporomoka katika utendaji wa kazi. “Suala la maadili kwa Watumishi wa Umma ni muhimu kufuatwa ili kuwa na utawala bora”, ameeleza

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dkt. Irene Isaka amesema kazi yao kubwa ni kusisitiza uadilifu katika ununuzi wa Umma, na kuhakikisha ukaguzi unafanywa kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu.

Dkt. Isaka ameeleza kuwa endapo manunuzi yatafanyika bila kufuata maadili kutakuwa na upotevu wa thamani halisi ya fedha na Serikali kukosa Kodi yake, amesema wanahakikisha manunuzi hayo yanafanywa kwa kufuata utaratibu wa Kanuni na Sheria zilizowekwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP Salum Hamduni akizungumza katika Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ambayo imeadhimishwa leo, Desemba 10, 2021 jijini Dat es Salaam.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi akizungumza katika Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ikiwa na Kaulimbiu ya Zingatia Maadili, Piga vita Rushwa, heshimu Haki za Binadamu ili kuimarisha Utawala Bora.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dkt. Irene Isaka  akizungumzia Maadili katika Ununuzi wa Umma kwenye Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...