Na Jane Edward, Arusha
RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dk.Edward Hosea amewataka wanasheria kufanya kazi kwa weledi wakutosha pamoja na kufata maadili ya kazi zao .
Amempongeza mwendesha mashitaka mashtaka mkuu wa serikali kwa kuweza kupunguza kesi mahakamani ambazo hazina ushaidi pamoja na kuchelesha usikilizaji wa kesi.
Ameeleza hayo wakati wa semina ya wanasheria iliyohusiana na kujikumbusha na anuai za kitaaluma ili kujua namna gani sheria zisadifiane na mikataba ya kimataifa kwa mfano ipo mikataba ya kimataifa ambayo sisi Tanzania tumekubali na Tumeanzisha sheria hapa nchini kusadifu izo sheria za kimataifa.
Amesema kunasheria nyingi ambazo zinatumika ikiwemo ya utakatishaji fedha.Pia semina hiyo pia itasaidia kuangalia namna gani sheria zetu zisishabiane na mikataba ya kimataifa ambazo serikali yetu tumezikubali hasa katika sheria ya utakatishaji fedha.
Aidha Dk. Hosea aliwasihi wanasheria nakuwaambia wakitaka kuishi kwa amani wazingatie maadili ya taaluma yao pamoja na kufuata sheria mbalimbali zilizowekwa.
Amesema utakatishaji fedha funzo la kwanza uwezi kuwa unatakatishaji fedha kama huja tenda kosa la kosa tangulizi kwa hivyo kunamashariti kabla ya mtu kabla ya kutiwa hatiani lazima vipengele ivyo viwe vimetendeka.
Kwa upande wake mmoja wawashiriki wa semina hiyo wakili Rogers Ntagara alisema umuhimu wa semina izi unawasaidia kuendelea kujifunza maana wanaamini katika kujifunza mambo mbalimbali ambavyo vinaenda na wakati kwa sababu pia sheria inabadilika kulingana na wakati.
Amesema kuwa kuna baadhi ya makosa ambayo yanakuja kutokana na mabadiliko ya kimtandao pamoja na teknojia kukuwa ivyo mafunzo hayo yatawasaidia sana katika kazi zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...