Baada ya kipindi cha kutokuwepo sokoni, kinywaji cha Smirnoff Ice Black sasa kimerudi sokoni huku kikielezea nia yake ya kuendelea kuunga mkono ukuzaji wa vipaji mbali mbali vya vijana wa Kitanzania

Kinywaji hiki ambacho kimechanganywa na Vodka na kilicho tayari kwa ajili ya kutumika, kilizinduliwa kwa mara nyingine jijini Dar es Salaam baada ya kutokuwepo sokoni kwa kipindi huku kikitoa fursa kwa wasanii mbali mbali kutoa burudani.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja uvumbuzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bertha Vedastus alisema pamoja na kuwaburudisha wateja wake na ladha nzuri na ya kipekee, kinywaji hicho pia kinajulikana kwa kuendeleza vipaji.

“Smirnoff Ice Black ni kinywaji kwa ajili ya kila mtu na pamoja na kuwaburudisha watumiaji wake, pia kimekuwa kikichangia katika kuibua na kukuza vipaji. Katika kipindi cha nyuma tumweza kufanya mashindano ya kutafuta Ma-DJ wakali na tulifanikiwa kufanya hivi mata tatu,” alisema.

Wakati kikirudi tena sokoni, Bertha alisema kinywaji hicho kitakwenda mbali zaidi kwa kuangalia vipaji vingine tofuati na Ma-DJ ili kuweza kutoa mchango mkubwa katika eneo hili ambalo limekuwa likisifika nalo.

Meneja uvumbuzi huyo aliwataka vijana wenye vipaji kuendelea kufuatilia kwa ukaribu taarifa mbali mbali kutoka Smirnoff ili kuhakikisha kuwa wanatumia fursa za kukuza vipaji zitakazo tangazwa.Hafla ya kutangaza kukirudisha sokoni kinywaji hicho ilifanyika jijini Dar jana

Wacheza muziki wa kikundi cha DWC dance cha jijini Dar es Salaam, wakitoa burudani safi kwa watuiaji wa  kinywaji cha Smirnoff Ice waliojitokeaza wakati wa halfa  Kampuni ya Bia ya Serengeti kutangaza kukirudisa tena sokoni kinywaji hicho.

DJ KG mmoja kati wa washindi wa kipindi cha nyuma wa shindalo la kusaka Ma-DJ lilikuwa linaendashwa na kinywaji cha Smirnoff akitoa burudani ya kupiga muziki wakati wa halfa kutangaza kurudi sokoni kwa kinywaji cha Smirnoff iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya wateja wa kinywaji cha Smirnoff Ice wakifurahia kinywaji hicho baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kukirudisha tena sokoni baaya ya kuwa hakipatikni kwa muda. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...