Malkia wa Muziki wa Singeli Snura Mushi akiwa ameambatana na Dragon Miongoni mwa aliowashirikisha katika EP yake"Jini" Huku akiwaomba Mashabiki kusikiliza Ep hiyo.


Na Khadija Seif, Michuzi TV

MALKIA wa Muziki wa Singeli Snura Mushi a.k.a Snura Majanga ameweka wazi kuwa bado hatamani wala kufikiria kumshirikisha Msanii mwenzake wa bongofleva Shilole.

Akizungumza mara baada ya kutambulisha rasmi EP yake "Jini" ambayo imebeba takribani nyimbo  5 ikiwemo Jini,naota,Kaliamsha, pamoja na Zaina  Huku akisindikiza na  Kaliamsha yenye maadhi ya Mtindo wa kisasa "Amapiano".

Hata hivyo Snura amefafanua zaidi kuwa amejipanga vizuri na Kwa Sasa anafikiria zaidi kujfanya kazi na watu waliomzidi kikazi hivyo hategemei Wala kufikiria kufanya kazi na Shilole kwani amemzidi kiuwezo.

Pia ameeleza Kwa namna gani ameweza kuufikisha Mziki wa singeli nje ya nchi na kuona Kwa jinsi gani baadhi ya Wasanii na watayarishaji wa Muziki kutoka nje na kumtaja Don jazzy kukubali Mziki huo wa Singeli.

Aidha, Snura amesema ndani ya Ep yake   imebeba Mafunzo mengi yenye kufundisha na kuelimisha hivyo amewataka  Mashabiki kuendelea kumpa ushirikiano wakutosha katika kupakua EP yake katika vyombo husika. Huku akisisitiza Mashabiki kukaa mkao wa kuipokea Albam yake ya kwanza kwani Yuko kwenye maandalizi ya kutayarisha Albam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...