Na Bakari Madjeshi, Michuzi Tv
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa suala la Mchungaji wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira linashughulikiwa kwenye Makao Makuu ya Jeshi hilo nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, ACP. Jumanne Muliro amesema kuwa suala hilo linaendelea kuchunguzwa katika Makao Makuu hayo, amesema hawezi kulizungumzia tena kwa kuwa lipo kwenye ngazi nyingine ya Jeshi hilo.
“Kijeshi Mamlaka iliyo juu kushughulikia jambo fulani, basi ndio yenye majibu kuhusu jambo hilo wanaloshughulikia na wao watatoa majibu kwa kuwa lipo huko”, amesema ACP. Muliro.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mchungaji huyo wa Kanisa la Efatha, Nabii Mwingira kudai kutishiwa kuuawa na baadhi ya Maofisa wa Serikali sambamba na kudai kupotea mali zake anazomiliki zenye thamani ya Shilingi Bilioni 10.
SUALA LA MSICHANA KUFANYA MAPENZI NA CHUPA ZA SODA
Katika hatua nyingine, ACP. Muliro amesema kuvuja kwa kipande cha ‘Video’ kilichomuonesha Msichana anayesadikiwa kuwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufanya mapenzi na Chupa za Soda, limefika katika Jeshi la Polisi na linaendelea na uchunguzi, amesema suala hilo litapelekwa kwenye Mamlaka zinazohusika pale uchunguzi huo utakapokamilika.
ACP. Muliro amesema hafahamu tuhuma za Msichana huyo na wengine kurubuniwa na baadhi ya watu kuvujisha ‘Video’ hizo kwa jamii, amesema uchunguzi unaendelea kwa Jeshi hilo na litapelekwa ngazi nyingine endapo uchunguzi huo utakapo kamilika.
SHEREHE YA MWAKA MPYA
Pia, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku fujo zinazofanywa na baadhi ya watu na badala yake limesisitiza kuimarisha usalama katika kuupokea mwaka huo wa 2022 ikiwa pamoja na kufanya ibada katika sehemu mbalimbali kwa amani na utulivu.
ACP. Muliro amesisitiza kuwa na vibali vya sheria kufanya Milipuko ya Baruti, Fataki ili kuimarisha utulivu na amani.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP. Jumanne Muliro akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa mbalimbali ikiwemo ya mkesha wa kuupokea Mwaka mpya wa 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...