Na Amiri Kilagalila,Njombe


MKUU  wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni amesema,kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu wananchi  12 wamejinyonga katika wilaya hiyo kwa sababu za wivu wa mapenzi,migogoro ya ardhi na ugumu wa maisha.

Kanoni amebainisha hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe, mhandisi Marwa Rubirya wilayani hapo.

Baadhi ya wananchi akiwemo Gisilary Nziku,Selest Mtega na Fred Ezekiel wamesema vifo vya kujinyonga vinachangiwa na msongo wa mawazo ambao unasababisha kuchukua maamuzi magumu na kuwepo washauri wenye umri mdogo kulingana na anaeshauliwa.

Aidha wananchi wamesema kutokomeza tatizo la watu kujinyonga serikali inatakiwa kuweka washauri wa umri tofauti pamoja na viongozi wa serikali za vijiji kumaliza tofauti za mwenye malalamiko kwa wakati pasipo kuchelewesha na kupendelea upande mmoja.

Mchungaji wa kanisa la TAG Melinze Cefania Tweve amesema chanzo cha kujinyonga ni kuwepo roho ya kishetani kwa maana imani za kishirikina na kuwa na uchungu na changamoto zinazojitokeza ikiwemo migogoro ya ndoa, ardhi na matatizo ya kiukoo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi wa polisi Hamis Issa ametaka wananchi kutojichukulia sheria za kujinyonga pindi inapotokea sintofahamu kati yao na kuomba wachungaji kuongeza kasi ya ushauri kwa wananchi ili kupunguza vifo vya kujinyonga Mkoani Njombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...