Na Pamela Mollel,Monduli
Tamasha kubwa la uhuru bonanza linalotarajiwa kufanyika Wilayani Monduli siku ya Jumamosi wiki hii maandalizi yake yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90
Wakizungumza na waandishi wa habari waandaaji wa Bonanza hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Costastine Shayo anasema tamasha hilo limeandaliwa na wadau wa michezo lenye lengo la kuibua vipaji pamoja na kusheherekea miaka 60 ya uhuru
Alisema kuwa mpaka sasa maandalizi ya bonanza hilo yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 ambapo yameshirikisha chama cha soka na chama cha riadha
Katibu chama cha Mpira wa miguu Monduli Abubakary Hamis alisema kuwa kupitia bonanza hilo litaweza kuitangaza vyema wilaya hiyo
"Hapa katika wilaya yetu ya monduli kuna watu mashuhuri ambao walishatumikia taifa hili lakini pia tuna vivutio vingi"alisema Hamis
Aliongeza kuwa bonanza hilo litaleta chachu katika michezo hasa kwa upande wa wanawake ikizingatiwa wilaya hiyo ni jamii ya kifugaji
Msemaji wa Bonaza hilo Amir Mongi alisema kuwa zaidi ya wadau wa michezo 3000 wanatarajiwa kushiriki Mashindano haya ambayo yatashirikisha mpira wa miguu,riadha, mbio za baskeli ,netbol,pamoja na kukimbiza kuku
"Bonaza hili nilakukata na shoka nawaomba wadau wapenda michezo wajitokeze kwa wingi"alisema Mongi
Mwenyekiti wa Uhuru Bonanza Costastine Shayo aliyekaa katikati akizungumzia maandalizi ya Bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika siku ya jumamisi wiki hii wilayani Monduli
Wa kwanza kushoto ni katibu wa chama cha mpira wa miguu Monduli Abubakar Hamis akiongea na vyombo vya habari juu ya bonanza kubwa linalotarajiwa kufanyika Monduli siku ya jumamosi wiki hii
Msemaji wa Bonanza Amir Mongi anasisitiza wadau kujitokeza kwa wingi kushiriki michezo mbalimbali
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...