Na Amiri Kilagalila,Njombe
KATIKA kuazimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara,wananchi wa kijiji cha Njomlole kata ya Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe wameshiriki maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya kijiji chao ili ujenzi uweze kukamilika kwa wakati na kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kwa kufuata umbali mrefu katika maeneo jirani.
Wananchi hao akiwemo Benito Mwalongo na Fred Mwageni wamesema kuwa wameona vema kujitoa katika kazi za maendeleo huku wakiomba serikali kuendelea kuunga mkono juhudi zao katika ujenzi.
“Nchi yetu imezidi kuwa na amani kwa muda mrefu nianaomba tu vijana tuendelee kujitokeza kwenye maendeleo na sisi leo ili kuadhimisha siku hii ya miaka 60 ya uhuru tumeona tushiriki kwa maendeleo kwasababu tumefurahi sana kupata fedha kwa ajili ujezni wa zahanati ili kupunguza changamoto ya kufuata huduma za afya umabli mrefu”
Naye afisa maendeleo ya jamii na ushirikishwaji wa jamii Atupewe Nauyo, amesema wananchi kwa sasa wamekuwa na mwitikio wa ushiriki kwenye maendeleo huku wakiomba wananchi kuendelea kuwa na moyo wakujitoa kwa manufaaa ya jamii.
“Kulingana siku hii ya uhuru tunajua mpaka sasa tumepiga hatua na mpaka hapa tulipofikia tunajua jamii imejua yenyewe inaanza kulingana na hitaji lao husika na ikifika sehemu Fulani serikali inakuja kusaidia,na leo tumefika na kuchangia nguvu zetu za ujenzi ili kuonyesha hapa tulipo tunaweza kufanya na serikali itatusaidia”alisema Atupewe Nauyo
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Jactani Mtewele,amesema kuwa kutokana na juhudi za wananchi katika ujenzi wa zahanati serikali imetoa fedha zaidi ya million 70 kwa ajili ya ujenzi huo huku akiwataka wananchi kuendelea kujitoa ili jengo hilo liweza kukamilika kwa wakati.
“Lakini sisi tumeamua kusheherekea kwa njia tofauti kidogo kwa kufanya kazi,wananchi wanahamasika kwasababu zahanati yetu mnayoiona hapa tayari tumeipata si chini ya milioni 70”alisema Mtewele
Wakati wanachi wa Njomlole wakiazimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara tangu ulipopatikana Disemba 9 mwaka 1961 kwa kushiriki ujenzi wa zahanati yao,kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa uhuru.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...