Na Denis Sinkonde-Songwe
MKUU wa mkoa wa Songwe Omary Mgumba amewapa siku tatu wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA wilaya ya Ileje kujieleza baada ya kubadili matumizi ya fedha bilioni 7 za ujenzi wa barabara ya kilimota saba kutoka mlima Kabulu yanapochimwa makaa ya mawe mpaka mgodi wa STAMICO uliopo Kiwira.
Mgumba amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa shughuli zinazofanywa na STAMICO katika uchimbaji wa makaa ya mawe kwenye mlima Kabulu uliopo kata ya Ikinga.
Nawapa siku 3 TARURA Ileje watoe taarifa ya kwanini wamebadili matumizi ya fedha bilioni 7 zilizotengwa na bunge kwa ajili ya ujenzi wa barabara inayotoka Kabulu, mto Mwalisi mpaka STAMICO Kiwira ‘‘alisema Mgumba”.
Mgumba amesema TARURA ileje wameiondoa kwenye mpango kujengwa barabara hiyo na fedha kuzielekeza kwenye barabara zingine wakitaka STAMICO wajenge kutokana na fedha za mapato yao ya ndani huku mkuu huyo wa mkoa akisema TARURA wamedharau maamuzi ya bunge kutenga bajeti hiyo muhimu.
Mgumba amesema bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania lilitenga bajeti ya fedha bilioni 7 kwa ajili ya kutambua umuhimu wa barabara hiyo ambayo ingerahisisha usafirishaji wa makaa yam awe kwani kwa sasa huzunguka umbali wa kilomita 38.
Kwa mkoa wa Songwe barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi wa Ileje, Songwe na taifa hivyo itakapokamilika itasaidia kuongeza uzalishaji wa makaa yam awe pamoja na kuongeza ajira ‘‘alisema Mgumba”.
Mgumba amesema ujenzi wa barabara hiyo uzingatie mahitaji kwani magari yenye uzito wa tani 30 yatapita kwa ajili ya kubeba makaa yam awe.
Samweli Andrew Kibarange mratibu wa shughuli za makaa yam awe kiwira amesema ujenzi wa barabara ya kilomita saba utakapokamilika utaleta tija katika shughuli za uzalishaji makaa yam awe na kuleta ushindani katika soko la dunia.
Kibarange alisema Serikali ihamasishe wamiliki wa viwanda vya saruji vya serikali na binafsi vya ndani na nje wanunue makaa ya mawe kutoka STAMICO kwani uzalishaiji wake huzalishwa kwa kiwango kinachohitajika ambapo kwa kipindi na kwa mwaka ujao wanatarajia kuzalisha zaidi ya tani milioni moja na laki tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...