Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani yaani International Civil Aviation Day (ICAD) iliyofanyika leo Desemba 07, 2021 ikiwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu Endelevu kwa Maendeleo ya Usafiri wa Anga Duniani”
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) yaliyopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza na watumishi, Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka hiyo, Teophory Mbilinyi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Hamza Johari amesema desturi ya sekta hii ya Usafiri wa Anga duniani ifikapo Desemba 07 kila mwaka huwa wanaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga hivyo kwa mwaka 2021 Mamlaka imetekeleza mambo mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho ya ICAD.
“Kuanzia Desemba 01 mpaka 03 TCAA kwa kutumia mameneja wa vituo 14 walienda redioni na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga, fursa zinazopatikana pamoja na kukinadi chuo chetu cha usafiri wa anga yaani CATC. Hivyo mameneja hao wameipeperusha vyema bendera ya TCAA kwa kueleza kwa kina masuala ya msingi ya Mamlaka hii” alisema Mbilinyi
Mbilinyi amesema Desemba 05 mwaka 2021 TCAA iliandaa mbio fupi zilizokuwa na jina “Fun Run” iliyohusisha watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), Shirika la ndege la Precision pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga hapa nchini.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza washiriki wote wa mbio hizo na kuwakumbusha kuwa kufanya mazoezi ni jambo la muhimu sana kwa sasa hasa ukizingatia yanasaidia katika kujikinga na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
Pia amesema Desemba 06 Mamlaka hiyo ilitoa msaada wa vitanda vya double decker 26 vitakavyohudumia wanafunzi 52 katika Shule ya Sekondari Azani na kusisitiza kuwa TCAA itaendelea kusaidia jamii kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika elimu na Nyanja nyingine za kijamii.
“Ili kuendelea kujikinga na UVIKO-19 TCAA tumeleta wataalamu wa afya kwa ajili ya kutoa chanjo ya UVIKO-19 kwa watumishi na nimearifiwa kuwa baadhi ya watumishi wamepatiwa chanjo hiyo hivyo nawaomba wale ambao hawajachanjwa kuchanja ili kuwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan aliyeonesha mfano kwa kuchanjwa hadharani”. Alisema Mbilinyi
Amewasisitiza Watumishi kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuweza kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory
Mbilinyi(kulia) akipanda mti pamoja na Mkaguzi Mkuu Kiongozi wa Usalama
wa Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Majaliwa Buruhani(kushoto) wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani ikiwa na kauli mbiu isemayo
“Ubunifu Endelevu kwa Maendeleo ya Usafiri wa Anga Duniani ” yaliyofanyika
leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka hiyo Ukonga-Banana jijini Dar es
Salaam leo. Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka hiyo, Teophory Mbilinyi
aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA) Hamza Johari.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory Mbilinyi akiwa kwenye picha ya pamoja Menejimenti ya Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani yaliyofanyika leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka hiyo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam leo.
Maandamano yakiendelea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani yaliyofanyika leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka hiyo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory Mbilinyi akipokea maadamano ya Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani yaliyofanyika leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka hiyo Banana jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...