Kampuni ya Tigo ambayo inadhamini mbio za km 21 za Kilimanjaro Marathon imetoa wito kwa washiriki wa mbio hizo waendelee kujisajili kwa wingi huku ikiwa imebaki takriban miezi miwili na nusu kabla ya kufanyika mashindano hayo maarufu Mjini Moshi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alitoa wito kwa washiriki watumie fursa hii ya punguzo la asilimia 20 kujisajili ili kuepusha usumbufu dakika za mwisho.

“Maandalizi yamepamba moto na usajili unaendelea tunawaomba watumie Tigo Pesa kujisajili kwa kubonyeza *149*20# kisha wataulizwa maswali machache ili kukamilisha usajili baada ya kulipia,” alisema  Woinde.

Aliendelea kusema kuwa Kwa mujibu wa waandaaji punguzo la bei litaendelea hadi Januari 7, 2022 ambapo bei zitapanda.

Alisema Tigo inaendelea na maandalizi vizuri ili kuwapa washiriki uzoefu kamili na kuhakikisha kuwa mbio za km 21 zinaendelea kuwa maarufu huku mbio za Kilimanjaro Marathon zikiadhimisha mika 20 mwakani.

“Huu ni mwaka wetu wa saba tangu tuanze kudhamini mbio hizi na msukumo mkubwa ni namna mbio hizi zinavyohamasisha utunzaji wa mazingira katika Mlima Kilimanjaro ili kuhakikisha theluji ya Mlima huo haiyeyuki, namna mbio hizo zinavyokuza vipaji, utalii na biashara kwa ujumla katika Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani,” alisema.

Alibainisha kuwa Tigo pia itaendelea na kampeni ya upandaji miti maarufu kama ‘Tigo Green for Kili.’

Wadhamini Wengine ni pamoja na Kilimanjaro Premium Lager-42km, Grand Malt-5km, wadhamini wa meza za maji ni Absa, Unilever, TPC Sugar, Simba Cement, Kilimanjaro Water, na wasambazaji maalumu Kilimanjaro Leather Industries Company Limited, GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel na CMC Automobiles.

Mbio za mwakani zitafanyika katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi Februari 27, 2022.

Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon huandaliwa na kampuni ya Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions Limited.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...