Na Khadija Kalili, Kibaha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakar Kunenge amewataka wakaazi wake kujitokeza katika kupata chanjo ya ugonjwa wa Uviko 19 kwa sababu wanaoathirika zaidi na ugonjwa huo ni watu ambao hawajapata chanjo.
Alisema kuwa hivi sasa nchi imepata dozi aina tatu ambazo ni Pfizer, Sinopharm na JJ huku muhusika atakua huru kuchagua aina ya chanjo kati ya hizo.
RC Kunenge alisema hayo leo Desemba 8 katika maadhimisho ya kusherehekea miaka 60 ya Uhuru wa nchi katika maadhimisho yaliyofanyika kimkoa kwenye Viwanja vya Mailimoja Kibaha.
RC Kunenge alisema kuwa maadhimisho haya yamefanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa kila Wilaya na Mikoa waaadhimishe sherehe hizo kimkoa huku kesho Desemba 9 itaadhimishwa kitaifa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Aidha Kunenge amewataka wananchi Mkoani hapa kutulia majumbani mwao na kufuatilia kwa ukaribu matangazo ya maadhimisho ya ilele cha shereke za miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika yatakayorushwa mubashara na vituo mbalimbali vya luninga huku akiwaeleza kuwa wanapaswa kuziingatia kuepuka misongamano isiyokuwa na ulazima ikiwa njia ya kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19 ambao bado haujapatiwa dawa duniani kote.
Katika maadhimisho hayo jambo lililovuta hisia za watu wengi ni kuwepo kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha wa Kwanza na kuhudumu kwa miaka kumi yaani kati ya mwaka 1978 hadi 1988 ambapo ni DC pekee aliyedumu kwa kipindi hicho wakati Wilaya hii ilipoanzishwa aliyetambulishwa kwa jina la Mary Francis Liwilo ambaye pindi alipopewa nafasi ya kuwasalimu wakaazi wa Kibaha alitoa historia ya Wilaya hiyo ambayo iliwavutia wengi.
Aidha sherehe hizo za Mkoa zilipambwa na bendi ya Ruvu JKT
Pia Kikosi Cha Karate cha Jeshi la Akiba kilinogesha sherehe hizo baada ya kuonyesha namna walivyoiva kimafunzo ya Ulinzi na Usalama huku wakiongozwa na mwanamama Rehema Dimwansi.
Wengine waluohudhuria sherehe hizo ni pamoja na viongozi wa dini, watu mbalimbali katika Mkoa wa Pwani pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya na Mkoa kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...