Na Mwamvua Mwinyi, Pwani


BAADHI ya wazee Mkoani Pwani, wameeleza kabla ya Uhuru kulikuwa hakuna shule ya Sekondari Wala shule ya awali ,ambapo ilitumika shule za kati ambazo zilikuwa Dar es salaam na zilichukua idadi ndogo ya wanafunzi kwenye mkoa huo hivyo kudidimiza sekta ya elimu.

Aidha Pato la mkoa limekua na kufikia Tirilioni 2.728 kwa mwaka 2019 tofauti na wakati tunapata Uhuru ambapo lilikuwa chini ya sh.milioni 70.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa Pwani ,bibi Mary Fransis Lwilo (77) ambae aliwahi kushika nafasi ya mkuu wa wilaya ya Kibaha ,alieleza kabla ya Uhuru mkoa haukuwa Kama ulivyo Sasa kiuchumi, kimaendeleo na ongezeko la watu na makazi.

Alisema ,watoto wa kike pia walikosa nafasi hizo ,Ni dhahiri kipindi hicho hakukuwa na tija inayoshuhidiwa Sasa.

"Siasa ndio kila kitu ,CCM ya toka Uhuru hadi Sasa ndio imesimama imara kuifikisha nchi ilivyo ,kwa mkoa huu Jiografia ilivyokuwa hakukuwa na idadi ya halmashauri Wala wilaya zilizopo Sasa ,Serikali imeunda wilaya na Halmashauri tunazoziona ,Ni hatua kubwa"alifafanua Bibi Mary.

Hata hivyo ,Mary aliuomba mkoa ,kukemea suala la vigodoro ambavyo vinarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kumkomboa mtoto hasa wa kike kwenye sekta ya elimu.

"Tupieni macho tatizo hilo ,Mimi naishi Visiga ,sifurahii kuona haya ,nimesoma nm,nimeshuhudia tulipotokea kielemu ,naelewa elimu ,nisingependa hii Hali ,napenda kuona mtoto wa kike anapiganiwa tusirudi kule tulipotokea "alibainisha Bibi Mary.

Akizungumza na wananchi katika maadhimisho hayo kimkoa ,mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema,mabadiliko kadhaa yametokea katika mkoa,kwani pato la mwananchi ni sh.milioni 2.106.121 kwa mwaka 2019 ukilinganisha na kipindi cha uhuru ambapo pato hilo lilikuwa chini ya sh.50,000.

Kunenge alieleza, kwasasa Serikali kuu kupitia Mamlaka ya mapato TRA inakusanya sh.bilioni 93.1 na Halmashauri zinakusanya sh.bilioni 38.056 kwa mwaka.

Kuhusu maji alisema, Hali ya upatikanaji wa maji kwa mijini imeongezeka kwa Sasa ni asilimia 84 na asilimia 72 kwa Vijijini.

Katika elimu idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 172 mwaka 1961 hadi 542 mwaka 2021 na shule za awali idadi ya wanafunzi walikuwa 0 mwaka 1961 na sasa imefikia 27,771.

"Tunawashukuru viongozi wote kwa awamu zote kwa kufikisha nchi ilipofika kiuchumi na nyanja zote."alisema Kunenge.

Akielezea sekta ya viwanda , Kunenge alieleza ,mkoa umetenga maeneo ya uwekezaji ya hekta 53,016 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ikiwemo EPZA hekta 9,800 .

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Sara Msafiri alisema ,wanaendelea kuwatumikia wananchi ili kupiga hatua kimaendeleo na kiuchumi na kuhakikisha wanaivusha Kibaha kutoka ilipokuwa na kukua zaidi inavyoonekana Sasa.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...