Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiendelea na zoezi la ukaguzi wa risiti za EFD katika malori ya mizigo yanayoelekea mikoa ya kusini katika eneo la Mwandege Wilaya ya Mkuranga,ambapo zoezi hilo lilianza tarehe 8 /12/2021.
Magari 21 yamekutwa na makosa mpaka kufikia leo tarehe 10/12/2021.
Meneja msaidizi wa Mkoa wa Pwani TRA Bw. Omar Chikwekwe alizungumza kwamba malori hayo yanavizia mida ya usiku kwa kuamini kuwa TRA muda wao wa kazi umeisha.
Kaika hatua nyingine Bw.Omari amewahimiza wafanyabiashara wenye malori, wenye viwanda na wafanyabiashara wanaouza bidhaa kutokukwepa kutoa risiti kwa manufaa ya Taifa letu.
Zoezi la ukaguzi linaendelea katika njia kuu zote zitokazo Dar es Salaam pamoja na Kariakoo.
Ofisa wa TRA Cosmass Mkinga (alievaa kitambulisho) akitoa maelekezo kwa mmiliki wa lori maeneo ya Mwandege Wilaya ya Mkuranga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...