MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud katika akizungumza kuhusu udhamini walioupata kutoka kwa Kampuni ya Ruby International inayojihusisha na uchumbaji madini kulia ni Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya na kushoto ni Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Thomas Machupa


Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Thomas Machupa akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud na kulia ni Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya



Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Thomas Machupa kushoto akimkabidhi kombe litakaloshindaniwa kwenye fainali ya Ligi ya Mkoa wa Tanga Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Said Soud kulia anayeshuhudia ni Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya


Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Said Soud kushoto akimkabidhi Kombe hilo Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya mara baada ya kukabidhiwa



NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud ameishukuru Kampuni ya Ruby International inayojihusisha na uuuzaji na uchumbaji wa madini nchini kwa kuona umuhimu wa kudhamini ligi ya mkoa huo.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Soud alisema udhamini huo utasaidia kuongeza ushindani na tija kubwa kwenye Ligi hiyo ambayo huchezwa kila mwaka .

Alisema licha ya udhamini huo kuongeza ushindani lakini pia utakuwa ni chachu ya kuibua vipaji vipya kwa vijana kupitia mpira wa miguu ambao baadaye kupitia timu za ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Alisema hatua ya kumpata mfadhili huyo ni jambo ambalo limeweka historia kwa soka la Tanga ambayo sasa inakwenda kukiinua chama hicho pamoja na kuboresha michuano hiyo .

“Lakini kikubwa niwashukuru kampuni hii ya Ruby International kwa kuona umuhimu wa kudhamini ligi hii hivyo niwahakikishie kwamba tutahakikisha tunashirikiana nao bega kwa bega”Alisema

Awali akizungumza katika Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Tom Machupa alisema watazidi kufanya mambo makubwa zaidi kwa ajili ya kukuza vipaji na kuipa hadhi ligi hiyo.

Machupa alisema wao kama kampuni ya Ruby watahakikisha wanashirikiana nao ili wazidi kufanya mambo makubwa kwenye Ligi ikiwa ni kukuza vipaji na kuipa hadhi ligi hiyo

Ligi hiyo inashirikisha timu 16 kutoka wilaya zote 8 za mkoa wa Tanga kila msimu ambapo msimu huu itakwenda kufikia tamati January 2, 2022 itakapochezwa fainali ya kumtafuta bingwa mpya wa mkoa.

Katika mchezo huo wa fainali timu ya Veterans tayari wameshaingia fainali wakimsubiri atakaye chuana naye kati ya Magomeni United na Pangani City ambao wanacheza nusu fainali kutafuta tiketi ya kuingia hatua hiyo.

Kwa msimu huu wa ligi ya mkoa 2021/2022 inayotarajiwa kufikia tamati January 2 mwakani,Kampuni ya Rubi International inayofanya shughuli za madini mkoani Arusha imetoa zawadi ya vikombe kwa timu itakayochukuwa ubingwa.
Zawadi nyengine zitatolewa kwa kocha bora,mchezaji bora , mfungaji bora pamoja na timu yenye nidhamu ambayo itapewa hati ya kutambuliwa kushiriki ligi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...