Mwenyeki wa Baraza la TEWW Dkt. Naomi Katunzi akihutubia wahitimu wa mahafali ya 57 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Sehemu ya wahitimu wa mahafali ya 57 ya TEWW wakifuatilia hotuba ya Mwenyeki wa Baraza la TEWW Dkt. Naomi Katunzi mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Michael Ng’umbi akieleza mafanikio ya Taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake wakati wa mahafali ya 57 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

. Mwenyeki wa Baraza la TEWW Dkt. Naomi Katunzi akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa mahafali ya 57 ya TEWW mwishoni mwa wiki.

(Picha na TEWW)

*************************

Na Mwandishi Wetu- TEWW

Wanafunzi 1505 wamehitimu masomo yao katika Taasisi ya Elimu ya watu Wazima (TEWW) mwaka 2020/2021 kati yao wanaume wakiwa 521 wanawake 984 kutoka katika kampasi za Dar es salaam, Morogoro na Mwanza.

Akihutubia wahitimu hao wakati wa mahafali yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyeki wa Baraza la TEWW Dkt. Naomi Katunzi amesema kuwa kati yao, wahitimu 443 ni wale waliosoma kwa njia ya kawaida na 1062 ni wale waliohitimu kwa njia ya Ujifunzaji Huria na Masafa kutoka katika Vituo 61 vya mafunzo.

“Ni imani yangu kuwa wahitimu wote mtakwenda kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi na bila shaka mtaenda kuongeza nguvu katika sekta ya elimu hasa katika Halmashauri mbalimbali”, alisisitiza Dkt. Katunzi



Akifafanua Dkt. Katunzi amesema kuwa TEWW imepanua wigo wa utoaji wa mafunzo katika ngazi ya Shahada kwa kutoa programu hizi kwa njia ya masafa ambapo alipongeza hatua hiyo na nkukukumbusha Menejimenti kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia taratibu za uendeshaji wa elimu kwa njia ya masafa.

Aidha, muendelee kuhamasisha jamii na wadau na kuzitangaza program zenu ili kuweza kupata wateja wengi zaidi na hatimaye kukabiliana na changamoto mliyoitaja awali ya kutokuwa na fedha za kutosha.

Aidha, Dkt. Katunzi aliwaasa wahitimu hao kuepuka uzembe, udanganyifu, rushwa na ufisadi kwani vitendo hivi havikubaliki hususan wakati huu wa Serikali ya Awamu ya Sita ya kipindi cha uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Michael Ng’umbi amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kuongeza idadi ya wasimamizi na wawezeshaji wa elimu ya watu wazima nchini kutoka 29 mwaka 1975 hadi kufikia wataalam takribani 12,800 waliohitimu programu mbalimbali za TEWW hadi sasa.

Halikadhalika, kutokana na uhitaji wa wawezeshaji wa elimu ya watu wazima,TEWW imeongeza Kampasi zake kutoka moja iliyopo Dar es salaam tangu kuanzishwa kwake hadi kufikia tatu.

Katika kuendeleza juhudi za kupanua wigo wa fursa za elimu na kuendelea kuongeza idadi ya wahitimu mwaka hadi mwaka, Dkt. Ngumbi amesema TEWW imeanza kutoa shahada kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa mwaka huu 2021/2022. Mafunzo haya ni kwa programmu za Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelezi na Elimu ya Watu Wazima na Maendeleo ya Jamii.

Mahafali haya ya 57 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika kampasi kuu ya Dar es Salaam yamefanyika mwishoni mwa wiki .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...