Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Marium Mwinyi (katikati) akikata Utepe kama ishara ya Ufunguzi wa Hoteli ya Tui Bluu Bahari Zanzibar iliyopo Kijiji cha Pwanimchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo alipofika rasmi kwa ajili ya kuifungua, akiwepo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Lela Mohamed Mussa (wa tatu kulia) pamoja na Viongozi wa Hoteli waliohudhuria hafla hiyo.[Picha na Ikulu] 11/12/2021.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitega Uchumi ZIPA Nd.Shariff Shariff (kushoto) akiwa pamoja na Wasaidizi wa Rais katika hafla ya Ufunguzi wa Hoteli ya Tui Bluu Bahari Zanzibar iliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi katika Kijiji cha Pwanimchangani Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja. [Picha na Ikulu] 11/12/2021.

Baadhi ya Viongozi na Wananchi walioalikwa katika Ufunguzi wa Hoteli ya Tui Bluu Bahari Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla iliyofanyika leo katika Kijiji cha Pwanimchangani Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja.[Picha na Ikulu] 11/12/2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akipokea zawadi maalum kutoka kwa Uongozi wa Hopteli ya Tui Bluu bahari Zanzibar katika hafla ya Ufunguzi wa Hoteli hiyo alipoufanya leo katika Kijiji cha Pwanimchangani Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja. [Picha na Ikulu] 11/12/2021.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipotambulishwa na kuwasalimiaViongozi katika Hoteli ya Tui Bluu Bahari Zanzibar na Mkurugenzi Mtendaji Reda Sweed (kushoto) iliyopo Kijiji cha Pwanimchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo alipofika rasmi kwa ajili ya kuifungua .[Picha na Ikulu] 11/12/2021. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi kwa kupokea saluti ya heshma mara alipofika katika Hoteli ya Tui Bluu Bahari Zanzibar iliyopo Kijiji cha Pwanimchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja alipofika rasmi kwa ajili ya kuifungua leo.[Picha na Ikulu] 11/12/2021. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Tui Bluu Bahari Zanzibar Bw.Reda Sweed (kushoto) pamoja na Mkuu wa wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohamed Mahamoud (kulia) na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Lela Mohamed Mussa (wa pili kulia) alipotembelea sehemu mbali mbali na kuangalia vyumba katika Hoteli Tui , mara baada ya kuifungua rasmi hafla iliyofanyika leo Kijiji cha Pwanimchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja. [Picha na Ikulu] 11/12/2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...