Na Atley Kuni, WAMJW, DSM.

Wananchi na wazazi wanaopata huduma kwenye kliniki ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemuomba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuongezewa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo.

Wakizungumza mbele ya Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima leo mara baada kufanya ziara ya kutembelea  kliniki ya watoto kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kuzungumza na wananchi na watoa huduma kisha kupokea maoni ya wazazi aliwaokuta wakipata huduma ndani ya kitengo hicho, wazazi hao wamemuomba yafanyike maboresho kwenye eneo la huduma za vyoo kwa ajili ya kuwasitiri watoto wadogo, kuwekewa feni ili upunguza joto kwa watoto wadogo, kuongezewa mabenchi ya kukalia.

"Mhe. tunaomba kuongezwa kwa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo kwani uhitaji mkubwa" alisema mmoja ya wananchi hao.

Kitengo hicho cha Mishipa ya fahamu pamoja na Ubongo, takwimu zinaonesha kinahudumia hadi Watoto 80 kwa siku, Idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na Idadi ya Mabingwa waliopo kwa sasa.

Akijibu maswali ya wananchi na wazazi hao Dkt. Gwajima alisema ameyapokea maoni na mapendekezo yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi.

"Ndugu zangu nimewasikia, uzuri hapa tupo na Mkurugezi anawasikia pia, lakini kama haitoshi, naomba niwape namba yangu ya kunitumia ujumbe mfupi, hii sio kwa ajili ya kupiga, niandikie ujumbe, tushauri nini tuweze kuboresha, kwa kutumia wataalam wetu tutachukua maoni yenu na tutayafanyia kazi” amesema Dkt. Gwajima.

Katika hatua nyingine, Waziri amemuelekeza Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyie kazi maboresho ambayo wananchi waliomba kuboreshewa, sambamba nakuendelea kuchukua maoni zaidi kwenye maeneo mbalimbali ambayo yatawasilishwa na wananchi ili huduma ziweze kuboreshwa.

Akizungumza wakati wa ziara, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Prof Laurence Museru aliahidi kuyafanyia kazi maboresho hayo, ambayo wananchi waliwasilisha ili kuweza kutatuliwa sambamba na kuongeza wataalam Bingwa wa masuala ya matatizo ya watoto ya Ubongo Pamoja na mishipa ya fahamu.

“Mhe. Waziri tumeyachukua haya ambayo wananchi wamewasilisha mbele yako, lakini mkakati mwingine tulionao ni kuongeza wataalam wabobezi kwa kuwapeleka shule ili wakihitimu waweze kusaidiana na hawa waliopo na kuondoa kabisa mapungufu haya ama kuyapunguza kwa asilimia kubwa. Prof. Mseru

Awali kabla ya kuwatembelea na kuzungumza wananchi hao waliofika kwa ajili ya huduma za kitabibu, Waziri Dkt. Gwajima, alifanya kikao cha Pamoja na Uongozi wa Hospitali hiyo kwa lengo la kukumbusha wajibu na kuweka mikakati ya uboreshaji wa huduma zinazo tolewa na Hospitali hiyo ya Taifa nchini.

Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Dkt. Dorothy Gwajima, Wakati wa Ziara yake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 29 Disemba, 2021, akimsaidia mmoja ya Mwananchi kuingiza namba ya.simu yakupokea Ujumbe mfupi kwenye Simu ya Mwananchi, ambapo pia alitoa namba hiyo kwa wananchi wengine na kuwataka kumuandikia Ujumbe mfupi pindi wanapopata changamoto ya huduma wanazopatiwa, au kushauri juu ya Maboresho ya huduma.
Dkt. Farhia Seif Ally, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto kwenye Mishipa ya kichwa pamoja na Ubongo, akimuelezea Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, jinsi wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Waziri huyo alipofanya ziara Disemba, 29, 2021
Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Dkt. Dorothy Gwajima, Wakati wa Ziara yake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 29 Disemba, 2021, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Prof. Laurence Mseru, wakati wa Ziara yake Hospitalini hapo 22 Disemba, 2021

Menejimenti ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakiwa wanamsikiliza Waziri Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Dkt. Dorothy Gwajima, Wakati wa Ziara yake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 29 Disemba, 2021, alipofika na kufanya nao kikao cha kuboresha hali ya utendaji kazi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...