Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wanunuzi na wasafirisaji wa Parachichi wameshauriwa Kujenga viwanda vya kusindika matunda hayo nchini hususani katika mkoa wa Njombe,ili kuongeza ajira kwa wazawa na kupunguza changamoto ya usafirishaji kwa kuwa kasi ya uzalishaji wa matunda hayo imekuwa kubwa ukilinganisha na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki
Wito huo umebainishwa katika mkutano mkuu wa wakulima na wadau wa zao la Parachichi mkoa wa Njombe chini ya asasi ya umoja wa wakullima,Njombe southern highland development association NSHIDA Pamoja na kampuni za ununuzi wa matunda ambapo mambo mbalimbali ya uwekezaji yamejadiliwa.
“Parachichi ya Njombe ni kubwa,ina mafuta mengi,na haina asidi kwa hiyo tushirikiane ili pia tuweze kununua matunda yote”alisema Eng.Martin Kayuni mkurugenzi wa kampuni ya Ecofly Tanzania inayojishughulisha na teknolojia ya kilimo
Frank msigwa ni mkurugenzi wa asasi ya wakulima mkoa wa Njombe NSHIDA amewataka wakulima kuzalisha matunda kwa kiasi ili waweze kumudu kuyahudumia mashamba yao.
“Inaongelewa kwenye majukwaa kama kilimo cha Parachichi ni kitu rahisi sana na imefika watu wanalima ekari nyingi na mwisho wa siku wakulima wanajikuta zile eka ziko porini na kilimo kimemshinda mkulima ni bora mkulima uanze kidogo kidogo unapozidi kujitanua” alisema Frank Msigwa Mkurugenzi wa Asasi ya Wakuima NSHIDA
Akizungumza afisa Umwagiliaji Mkoa wa Njombe ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo mkuu wa wakulima mkoa wa Njombe amewataka wawekezaji kuja nchini kuwekeza kwani kuna mazingira rafiki ya uwekezaji.
“Utakuta wafanyabiashara mnafuata Matunda huku halfau kiwanda kipo huko,kwanini hicho kiwanda msikilete Njombe,leteni kiwanda chenu Njombe na serikali ipo tayari kuweka mazingira mazuri kwasababu sera zetu Tanzania ni kuwa na viwanda,karibu mlete Viwanda ila hawa wakulima walete matunda yao karibu”alisema Braison Mjanja Afisa Umwagiliaji mkoa wa Njombe.
Frank Msigwa mkurugenzi wa asasi ya wakulima mkoa wa Njombe NSHIDA akizungumza na wakulima wa parachichi katika mkutano huo wa wakulima uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani Motel uliopo mjini Njombe
Baadhi ya wakulima waliofika kwenye mkutano wa wakulima wa parachichi mkoani Njombe.
Moja ya miti ya matunda ya Parachichi yanayolimwa na wakulma hao mkoani Njombe.
Baadhi ya wakulima waliofika kwenye mkutano wa wakulima wa parachichi mkoani Njombe.
Moja ya miti ya matunda ya Parachichi yanayolimwa na wakulma hao mkoani Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...