Na Mwandishi Wetu
KWA mwaka wa tatu mfululizo wanafunzi wa kike wamewapiku wavulana na kuongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za wanafunzi bora katika Chuo Kikuu Ardhi (ARU).

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Gabriel Kassenga wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao kabla ya mahafali yanayofanyika siku ya Jumamosi.

Jumla ya tuzo 135 zilitolewa kwenye hafla hiyo na kati ya tuzo hizo, 74 ambazo ni wastani wa asilimia 54.8 ya zawadi zote zimechukuliwa na wasichana na 61 ambazo ni asilimia 45.2 zimechukuliwa na wavulana.

Alisema ingawa idadi ya wasichana chuoni hapo ni asilimia 40 lakini wamekuwa wakifanya vizuri na kutwaa tuzo hali ambayo inadhihirisha kwamba wasichana wanauwezo wa kufanya vyema kwenye masomo ya sayansi kinyume na fikra za baadhi ya watu.

“Katika ushindi wa jumla wanafunzi wawili wamefungana kwa alama ambao ni msichana na mvulana hivyo utaona kwamba wasichana wamepata tuzo nyingi kuliko wavulana ingawa kwa idadi wasichana ni wachache hapa chuoni kulinganisha na idadi ya wavulana,” alisema

Aliwapongeza wanafunzi wote waliopokea tuzo hizo na kuwasihi waendelee kusoma kwa bidii ili waje kuwa mfano wa kuigwa na wanafunzi wenzao na jamiikwa ujumla.

“Napenda kuwapongeza wanafunzi wahitimu kwa kujinyakulia tuzo mbalimbali na wengine wamekuwa wakitwaa tuzo kama hizi kwa miaka yote wakiwa chuoni hapa hii inamaanisha kwamba kwenye juhudi ya kweli mafanikio hupatikana,” alisema

Alisema sherehe hizo ambazo hufanyika kila mwaka ni muhimu kwani hutoa hamasa kwa wanafunzi wa chuo hicho ili waendelee kuweka juhudi kwenye masomo na hatimaye waweze kupata ufaulu wa juu.

Profesa Kassenga alisema sherehe hizo zimekuwa zikiwezeshwa na wadau mbalimbali kwa kujitolea ufadhili wa hali na mali kwa wanafunzi waliofuzu kupata tuzo hizo na aliwaomba wasichoke kuwasaidia kufadhili tuzo hizo.
Alisema zawadi mbalimbali zinazotolewa na wafadhili hao zimekuwa zikiwasaidia wanafunzi hao kuongeza mitaji na utendaji kazi mara wanapomaliza masomo yao.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa, akimkabidhi tuzo msichana aliyefanya vizuri zaidi kwenye masomo ya mwaka 2020/21 kwa wasichana, Grace Mhina wakati wa sherehe za kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zilizofanyika chuoni hapo siku ya Ijumaa. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia taaluma, Profesa Gabriel Kasenga.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa, akimkabidhi tuzo mvulana aliyefanya vizuri zaidi kwenye masomo ya mwaka 2020/21 kwa wasichana, Grace Mhina wakati wa sherehe za kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zilizofanyika chuoni hapo siku ya Ijumaa. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia taaluma, Profesa Gabriel Kasenga.


Viongozi wa meza kuu wakiwa wamesimama kwaajili ya kuanza zoezi la kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye hafla ya kuwatunuku wanafunzi bora wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), ambapo jumla ya tuzo 135 zilitolewa na kati ya hizo 74 kuchukuliwa na wasichna na 61 wavulana.
Baadhi ya washiriki wa sherehe za kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zilizofanyika chuoni hapo Desemba 3,2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...