Na.Vero Ignatus,Arusha
Katika kuadhimisha kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limesema kuwa katika kipindi cha miezi miwili kuanzia Oktoba hadi Novemba 2021 kesi zilizoripotiwa kwenye vituo vya Polisi Wilaya zote za Mkoa wa Arusha ni 693,ambapo watuhumiwa waliokamatwa ni 702 ambapo wanaume ni 419 na wanawake ni 283 katika makosa yanayohusu ukatili
Hayo yamesemwa na Afisa Mnadhimu namba moja ACP Mary Kipesha kwamba jumla kesi ambazo zimeshinda mahakamani ni 54 na watuhumiwa 284 walikutwa na hatia ambapo wanaume ni 206 na wanawake 78 na wamehukumiwa vifungo mbalimbali kila mmoja kutokana na makosa yaliyowatia hatiani ambapo Jeshi hilo limeendedelea kufungua madawati ya kusiliza kesi za ukatili wa kijinsia katika vituo mbalimbali vya Polisi,
Kumlazimisha mtoto mdogo kuolewa kabla ya umri wake ni ukatili,vitisho vya aina yeyote unavyoviona kwa mtu anayekuzudi nguvu vyote hivyo ni ukatili tuvikomeshe,na kuvitokomeza,vilevile tunasisistiza elimu iendelee kutolewa, Kwa kuendelea kutoa elimu katika jamii yetu tumepunguza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia .''alisema Kipesha
Kipesha ametoa wito kwa makundi yote na taasisi za serikali, kidini na zisizo za kidini kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa Elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia na watoto ambao umekuwa ukizolotesha ustawi imara wa jamii yetu. Sambamba na hilo niwaombe wananchi kuendelea kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia na watoto katika jamii inayowazunguka ili kulisaidia Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kumaliza kabisa vitendo vya kikatili katika Mkoa wetu wa Arusha.
Vilevile amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia dawati la jinsia na watoto ,kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali na za kiraia limeendelea kutoa elimu kwa makundi yote juu ya ukatili wa kijinsia, taasisi hizo ni HAKI KAZI CATALYST, CWCD, TCYLO, FAE, AVUREFA, PWC, PINGO FORUM.
Hata hivyo amesema licha ya kuwa na changamoto kwa baadhi ya jamii kuto toa ushirikiano wa utoaji wa taarifa za ukatili wa kijinsia na watoto katika maeneo yao, Jeshi la Polisi limendelea kutoa elimu kwa jamii na makundi yote ambapo hivi sasa matokeo chanya ya mabadiliko hayo, yameanza kuoneakana na kupelekea kuongezeka kwa kuripotiwa vitendo hivyo katika madawati yalipo katika vituo vya Polisi Mkoa wa Arusha.
Wakati huo huo amefungua dawati la Jinsia na watoto katika wilaya ya kipolisi Murieti iliyopo katika Jiji la Arusha ,ambapo amesema kwa kitendo hicho kesi zote za ukatili wa kijinsia zitasikilizwa kwa umakini mkubwa
Badhi ya Akari wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe katika kilele cha siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia usemao ''Zuia ukatili dhidi ya watoto''

Maandamano yakiendelea kama inavyoonekana katika picha ikiwa ni kilelel cha maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo ''EWE MWANANCHI KOMESHA UKATILI SASA ''
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...