Na. Victoria robert
Waziri wa mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema serikali ya Tanzania bado inalitambua soko kuu la kimataifa la Kasenda kuwa ni miongoni mwa masoko matatu ya kimataifa ambayo yanatumika kutoa vibali ili kuhakikisha mazao ya samaki yanayopelekwa katika mataifa mengine yanakuwa katika ubora wa hali ya juu.
Waziri Ndaki ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kuongea na wananchi na wafanya biashara katika soko la kimataifa la Kasenda lililopo kata ya Muganza wilayani hapa. "Tanzania tuna masoko matatu tu ya kimataifa, soko la samaki la Feri lililopo Dar es Salaam, Soko la Kirumba lilolopo jijini Mwanza na Kasenda lililopo Chato.
'' Nataka niwahakikishie soko lenu la Kasenda lipo pale pale na lipo kimkakati chini ya Wizara ya Mifugo na uvuvi, halikuletwa hapa kwa bahati mbaya" alisema mhe. Waziri Ndaki.
Waziri Ndaki amesema masoko mengine yanayotajwa na baadhi ya watu hayapo na Wizara haiyatambui kwani masoko hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...