Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amempa mamlaka Katibu Tawala za Mkoa wa Singida kusainia malipo ya mafundi wanaojenga Kituo cha Afua Ilunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

Mhe. Ummy ametoa maamuzi hayo wakati yake ya kukagua miradi yab maendeleo katika Halmashauro hiyo na kufika kwenye Kituo cha Afya Ilunda ambacho kiko nyuma kwenye ujenzi kwa sababu ya mivutano ya Baraza la Madiwani katika Halmashauri hiyo.

‘Nimeambiwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hii anakataaa kusaini mikataba ya ujenzi sababu tu hajaafiki kituo hiki kijengwe Ilunda na hata kazi hii kuchelewa kuanza ni kwa sababu ya mivutano hiyo mpaka TAMISEMI kuingilia kati na kutoa maelekezo’

Sasa kama mnakataa kusaini Milataba Mamlaka hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida apitishe Mtakaba wa ujenzi ili kazi iendelee na ujenzi uweze kukamilika kwa wakati alisisitiza Ummy.

Mivutano yetu haiwasaidii wananchi wanachotaka kuona ni maendeleo tu sasa Kila diwani akitaka Kituo kikajengwe kwenye Kata yake haiwezekani Vituo hivi vinajengwa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

Aliongeza kuwa maslahi ya viongozi yasikwamishe utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa sababu Serikali inaleta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi lakini baadhi ya viongozi wanatanguliza maslahi yao mbele badala ya kuzipa kipaumbele changamoto zinazowakabili wananchi hili halileti Afya kwenye Halmashauri zetu’ alisisitiza Mhe. Ummy.

Mhe. Ummy alihitimisha kuwa maslahi binafsi ya viongozi wetu kwa namna yeyote ile yasikwamishwe utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa tuzingatie maslahi mapana ya wananchi.

Akitoa ufafanuzi katika Kituo hicho cha Ilunda Mkurugenzi wa Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na Lishe toka OR-TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe amesema halmashauri ya Wilaya ya Mkalama iliwasilisha mahitaji ya kuomba Fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho mwezi February,2021 na fedha ilipopatikana ndipo wakakipa kipaumbele kituo hicho.

Pia alieleza vigezo vinavyotumika katika uteuzi wa maeneo ya kujenga vituo vya Afya ni Idadi ya watu, umbali kutoka Kituo kilichopo cha kutolea huduma pamoja na wingi wa magonjwa hivyo sio kila Kata inapata Kituo ila zinapata zile tu zilizokodhi vigezo hivyo.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya hicho Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Dkt.Ibrahim Pazia amesema fedha za ujenzi zilifika Agosti 05,2021 lakini maamuzi ya wapi kijengwe kituo hicho ndicho kilichochelewesha kuanza sambamna na vifungu vya matumizi ya fedha hizo.

Kituo cha Afya Ilunda kilipokea sh. Mil 250 kutoka katika Tozo ya miamala ya simu na fedha hizo zitajenga majengo matatu ambayo ni Jengo la wagonjwa wa Nje, maabara pamoja na kichomea taka.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...