Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Afisa Madini Mkazi na Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha wanafungua Soko la Madini wilayani Bunda Mkoa wa Mara ili kuwarahisishia wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kupata huduma hiyo karibu.

Agizo hilo amelitoa leo Desemba 28, 2021 wakati akizungumza na wachimbaji katika eneo la Kinyambwiga lililopo Kata ya Guta wilayani Bunda mkoani Mara.

Dkt. Biteko amesema kuwa, haiwezekeni mchimbaji ana dhahabu yake mfukoni anaenda hadi Musoma kutafuta soko.

Amesema, ni lazima soko la madini lianzishwe Bunda ili watu wafanye biashara ya madini kwa urahisi.

"Natoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya, Afisa Madini na Katibu Tawala wa Mkoa ambaye kwa mujibu wa kanuni ya uanzishwaji wa masoko ya madini ndiye mwenye kutafuta eneo sahihi ya kuweka soko la madini," ameongeza Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, bado kuna umbali mkubwa hivyo kutoka eneo la machimbo mpaka Bunda na kuwataka kianzishwe kituo kidogo cha kununua madini katika eneo la Kinyambwiga. Amesema, eneo litaandaliwa kwa wafanyabiashara wa madini ( Brokers) ili biashara yote ifanyike katika eneo hilo la wachimbaji.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...