Na John Walter-BabatiWatu wasiofahamika wamevamia nyumba ya mchungaji na kuiba nyaya za umeme na kuharibu mfumo mzima wa umeme (wire ring)uliokuwa umewekwa katika nyumba hiyo katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Komoto mjini Babati.

Nyumba hiyo ya Mchungaji ipo katika hatua za mwisho za umaliziaji kabla ya mchungaji kuhamia.

Hayo yamebainishwa leo na Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo usharika wa Komoto Mchungaji Godlsten Mkenda katika ibada iliyofanyika leo Jumapili Desemba 12 kanisani hapo.

Kutokana na tukio hilo kiongozi Mchungaji Godlsten Mkenda ameongoza maombi maalum yaliyofanywa na waumini wa kanisa hilo kuwaombea kwa Mungu waliotenda uhalifu huo wa kutwaa mali isiyo yao ili waokoke na kumrudia Mungu.
Hata hivyo mchungaji Mkenda aliwataka waumini watoe taarifa pindi wanapopata taarifa za waliohusika na tukio hilo.

Mchungaji Mkenda amesema "katika roho ya Kikristo, tunaomba kila mmoja aliyehusika kuguswa na Roho Mtakatifu na kurudisha nyaya hizo"


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...