Akitangaza
washindi wa droo hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki, Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Bi. Agnes
Kaganda, alisema jumla ya washindi 6 walipatikana kupitia droo hiyo na
kujishindia zawadi ya shillingi million sita fedha taslimu.
“Katika
droo ya leo jumla ya washindi sita (6) wamepatikana ambao ni Manish
Govindji, Abdulkarim Lema, Emashu Investment, Paul Kadonya, Emile
Singano, Ibrahim Nyange na Pritipal Chadha na hivyo wameweza kujishindia
zawadi za fedha taslimu kiasi cha sh mil 6. ” alitaja
Washindi
hawa sita kwa mujibu wa Bi Kaganda watakabidhiwa zawadi zao katika
maeneo yao waliopo huku akibainisha kuwa benki hiyo itaendelea na droo
kama hizi kila mwezi na washindi wataendelea kuingia kwenye droo
itakayowawezesha kushinda zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard.
“Wateja
wetu wa sasa na wale wapya watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi
hizi kila watakapojiwekea akiba ya kuanzia Tsh. 500,000 na kuendelea.
Kadili wanavyojiwekea amana kubwa zaidi ndivyo wanavyojiweka kwenye
nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi,’’ alisema Bi Kaganda wakati wa
droo hiyo iliyohudhuriwa pia na muwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha nchini.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo Bi
Kaganda alisema inalenga kuleta mabadiliko kwenye mtazamo wa uhifadhi wa
amana miongoni mwa watanzania kutoka kuhifadhi pesa majumbani na badala
yake wazihifadhi kupitia benki hiyo kwa usalama wa fedha zao sambamba
na faida nyingine nyingi ikiwemo riba.
“Lengo si tu kuhamasisha
watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea amana, tunachohitaji ni kuona
kwamba Watanzania wengi wanajiwekea amana zao sehemu salama ili
kujiendeleza kukua kiuchumi ndio maana tumejipanga kuwahamasisha watumie
akaunti zetu mbalimbali ikiwemo akaunti ya mshahara inayotumika kwa
matumizi mbalimbali ya kila siku,’’ alitaja.
Alitaja akaunti
nyingine kuwa ni pamoja na akaunti ya mzalendo inayoendeshwa bila makato
ya kila mwezi, akaunti ya haba na haba, akaunti ya faida ambayo
inakuruhusu kuweka akiba na kupata riba pamoja na akaunti ya Nyota
ambayo ni akaunti maalum kwa ajili ya Watoto pamoja na akaunti ya
wajasiriamali inayowahudumia wafanyabiashara na mahitaji yao tofauti
tofauti ya kibiashara.
Kwa upande wake Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Bi Neema Tatock alitoa pongezi kwa washindi wa promosheni hiyo huku akiwahamasisha walengwa kushiriki kwa wingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata huku akiwahakikishia kuwa Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha zoezi la kupata washindi linafanyika kwa kwa uwazi na kwa kufuata misingi halali ya kubahatisha.
Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda, (Katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa zoezi la uendeshaji wa droo ya kuwatafuta washindi wa droo ya pili ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana kupitia benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Neema Tatock (Kulia) na Meneja Msaidizi wa Bidhaa za Rejareja kutoka benki hiyo, Callist Butunga (Kushoto)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...