Adeladius Makwega,Dodoma
Katika matini yangu
iliyotangulia juu ya Kabila la Wasumbwa msomaji wangu unakumbuka nilivyokusimulia
utani baina ya Wasumbwa, Wazaramo na Wagogo na namna Wagogo walivyoshiriki
kuuvamia msafara ya Chifu wa Wasumbwa Kafuku na kumuua na hata mwisho
nilimalizia madhara yaliyowapata Wagogo hadi walipofunga safari hadi Kahama kwa
ndugu wa Chifu Kafuku kuwaomba msamaha kwa tukio hilo.
Unakumbuka msomaji wangu pia
nilisimulia namna Wagogo walivyotakiwa kutoa fidia ya mifugo 300 na hapo ndipo
msamaha ulikubaliwa na ndugu wa Chifu Kafuko kufika Dodoma na kuichukua pembe
iliyokuwa ikisababisha ukame na njaa katika makaazi ya Wagogo na kuichoma moto.
Kwa msomaji wangu, naomba
ukumbuke kuwa Wasumbwa kama walivyoelewana sana na Wazaramo kwa kuwafafanisha
na Wanyamwezi kumekuwa na hoja moja kubwa mbili, Lugha ya Kisumbwa inalingana kwa
karibu na Kinyamwezi na pia Wasumbwa kuna wakati waliaminika walikuwa chini ya
Chifu Mirambo. Ndani ya hilo kuna hoja kuwa na hata maandiko machache mno
yaliyoandikwa juu ya kabila hili na machifu wake, kw ahiyo halifahamiki sana.
Wazaramo waliwatazama
Wasumbwa kama Wanyamwezi kwa kuwa walikuwa wakitokea eneo ambalo ndilo
Wanyamwezi wakitokea .”Twekupuna eyo kupunila mwezi.” Ikimaanisha kuwa
tunatokea huko unakotokea mwezi (Wanyamwezi)-Those who produce moon.
Wasumbwa wana kitu tofauti
na makabila mengine hasa suala la mahusiano baina ya binamu wa kike na wakiume,
hawa huwa ni ndugu kabisa yaani kaka na dada na hakuna mahusiano ya kimapenzi
wala kuoana baina yao. Hawa wanaheshimiana kabisa kama kaka na dada wanaozaliwa
tumbo moja, ndiyo kusema mtoto wa mjomba na shanganzi hawawezi kuoana.
Wasumbwa wana utani kama
nilivyokujulisha na Wazaramo, Wagogo, Wanyamwezi na na pia na Wangoni, pale
mtani wao anapofariki hali ya utani huwa mara dufu kwa kusema kuwa “Tukulya mno
bwalelo.” Kwamba leo tutakula mno, kwa kuwa mtani amefariki, hali hii ya utani
inaweza pia kuwapo kati ya koo na koo za Kisumbwa zenyewe.
Wasumbwa kama yalivyo makabila
mengine na wao ni mabingwa wa kutambika na ya siku ya kutambika huwa wanaandaa
pombe ya tambiko ambapo kwa wale watani siku ya tambiko hilo uibuka na
kuichukua pombe ya tambiko na kuinywa bila ya kuogopa madhara yoyote
yatakayotokea kwao kwani pombe ya tambiako huwa inaheshimika sana kwa ajili ya
mizimwi. Mtani anaweza kufika wakati wa tambiko akaichukua na kuinywa huku
akisema kuwa “Misamba yilabafile hi?.” Hivi nyie haya matambiko mnadhani
yatawafikisha wapi?
Hapo juu nilikujulisha kuwa
kabila lingine lenye utani na Wasumbwa ni Wangoni, kama ilivyo desturi Wangoni
walikuwa mabingwa wa vita na ukitazama makabila mengi yana utani na Wangoni, kwa
hiyo hilo limefanya hata Wasumbwa kuwa na utani na ndugu hawa ikiaminika kuwa
Wagoni walipokuwa wakipigana waliwahi kufika eneo la Busumbwa na hapo ndipo
utani ukaanza. Wasumbwa kwa Wangoni wanatazamwa kama“Bafu bakadeni.”
Ikimaanisha watu wa kuuwawa tu. Mtu wa namna hiyo ni sawa na mtumwa. Utani huo
na kivita ulisabisha kukawepo na urafiki mkubwa wa Wasumbwa na Wangoni.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...