Serikali imeitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakati wa utelekezaji wa majukumu yao kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali kwa maslahi mapana ya Taifa.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande (Mb) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano-APC Bunju jijini Dar es Salaam.
“Hii Bodi kazi yake kubwa ni kuweka sera na mikakati itakayoiongoza na kuishauri Menejimenti katika kutekeleza majukumu ya Taasisi kwa kuzingatia sera za serikali katika kutoa huduma kwa wananchi” alisema Chande.
“Ni matarajio ya Serikali kwamba mtafanya kazi yenu kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu kwa maslahi mapana ya Taifa letu”alisema Chande.
Aidha aliwataka wajumbe wa Bodi kutumia vitendea kazi walivyopewa ikiwemo nyaraka mbalimbali zenye maelezo ya majukumu ya Bodi na Taasisi zinavyofanya kazi ili iwe rahisi wakati wa utekelezaji wa majukumu.
“Nimesikiliza maelezo ya Mtendaji wa NBAA, nimeweza kufahamu japo kwa uchache kuhusu majukumu ya Taasisi yetu ya NBAA kwa kuzingatia kuwa nami nimeteuliwa siku za hivi karibuni kushika wadhifa huu wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango”, alisema Mhe. Chande.
Aliongeza kuwa atafanya ziara rasmi za kuzitembelea Taasisi zote zilizo chini ya wizara ikiwemo ya NBAA ili kufahamu kwa undani majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Taasisi za Wizara ya Fedha na Mipango.
Chande
aliitaka Bodi hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuisimamia NBAA
kwa mustakabali wa kada za Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ambao ni
muhimu katika kusimamia rasilimali fedha.
Natoa pongezi binafsi kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kukuteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, nawapongeza pia wajumbe wote 11 wa Bodi ya NBAA mlioteuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA, CPA Prof. Sylivia S. Temu alisema wapo tayari kufanya kazi na kuahidi kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia taaluma ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini.
Prof. Temu alimshukuru pia Mhe. Rais kwa kumuamini na kumteua kusimamia Bodi hiyo na kuahidi kuwa watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa na Serikali ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Pius Maneno, alimshukuru Naibu Waziri kwa kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA.
CPA Maneno, alimuahidi Mhe. Chande kuwa Taasisi hiyo itaipa ushirikiano wa kutosha Bodi ya Wakurugenzi walioteuliwa ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande (Mb),
akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), uliyofanyika
katika ukumbi wa Mkutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu Tanzania (NBAA), Prof. Sylivia S. Temu, akizungumza wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliyofanyika katika Kituo cha Mikutano
APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania
(NBAA) CPA Pius Maneno akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi
hiyo uliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa APC Bunju jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande (Mb), akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Prof. Sylivia S. Temu wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa
APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa
anazindua Bodi hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa APC Bunju jijini Dar es
Salaam.
Mkutano
ukiendelea wa halfa ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa
ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), uliyofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande (Mb) akiwa katika
picha ya pamoja na Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), mara baada
ya kuizindua rasmi Bodi hiyo. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi NBAA, Prof. Sylivia S. Temu na kushoto kwa Naibu
Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno.
Natoa pongezi binafsi kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kukuteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, nawapongeza pia wajumbe wote 11 wa Bodi ya NBAA mlioteuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA, CPA Prof. Sylivia S. Temu alisema wapo tayari kufanya kazi na kuahidi kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia taaluma ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini.
Prof. Temu alimshukuru pia Mhe. Rais kwa kumuamini na kumteua kusimamia Bodi hiyo na kuahidi kuwa watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa na Serikali ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Pius Maneno, alimshukuru Naibu Waziri kwa kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA.
CPA Maneno, alimuahidi Mhe. Chande kuwa Taasisi hiyo itaipa ushirikiano wa kutosha Bodi ya Wakurugenzi walioteuliwa ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...