MKUU wa Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Jokate Mwegelo ameshiriki katika hafla ya makabidhiano ya Madarasa mapya 157 yaliyojengwa katika Shule 24 za Sekondari iliyofanyika leo Januari 3, 2022 katika Shule mpya ya Sekondari Dovya iliyopo Kata ya Chamazi wilayani humo.

Katika hafla hiyo Jokate amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha fedha Sh.Bilioni 3.14 za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa, na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa hayo.

Ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ulioanza Novemba 1, mwaka 2021 na kukamilika Disemba 31, 2021 na kukamilika na kukabidhiwa kwa madarasa hayo  vitakavyoondoa changamoto ya madarasa kwa muhula wa masomo wa mwaka 2022.

Akizungumza leo wakati wa tukio la Makabidhiano ya madarasa hayo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo ametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo Temeke inamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zimekwenda kutatua changamoto ya masomo ,hivyo msimu wa masomo wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato Cha kwanza wote watakwenda shuleni.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza ushirikishwaji wa wananchi katika miradi inayotekelezwa na serikali, ili kuwafanya kutambua matumizi ya mapato yanayokusanywa na halmashauri yao kwa maendeleo ya Temeke, huku akitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wafike shule kwa wakati, kwa sababu madarasa hayo yamejengwa kuimarisha elimu ya sekondari nchini.

“Miradi yote ya maendeleo lazima tushirikishe Wananchi ili wajionee 'laivu' bila chenga, tutaendelea kuwashirikisha Wananchi kuanzia miradi inapoanzishwa, inapoendelea, inapokamilika, mapato, matumizi na hata kwenye uzinduzi kuwaomba wawepo ili kuona kwa vitendo na sio kusimulia tu” amesema Jokate 

Aidha ametoa mwito kwa viongozi wa bodi za shule za Sekondari kuendelea kukaa vikao kazi muhimu, ili kuendelea kujadili namna bora ya usimamizi wa shule, kuinua maendeleo ya elimu, na kukuza viwango vya ufaulu wa wanafunzi ili kuipaisha Wilaya ya Temeke katika ramani bora ya elimu nchini.

Ameongeza ni vema akatoa shukrani kwa Meya, Naibu Meya , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ,Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa wakati wote wa kutekeleza miradi ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa madarasa hayo huku akiwashukuru pia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa usimamizi wao wa kusimamia miradi ya maendeleo ya wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo akizunguma leo Januari 3,2022 wakati wa tukio la Makabidhiano ya madarasa  157 kwa shule za sekondari zilizopo katika Wilaya hiyo.Fedha ambazo zimetumika katika ujenzi huo ni zaidi ya Sh.bilioni tatu ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kutatua changamoto ya upungufu wa madarasa kwa shule za sekondari.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Elihuruma Mabelya(Kushoto) wakati wa tukio la Makabidhiano ya madarasa ya Sekondari 157 yaliyojengwa katika Wilaya hiyo.Fedha za ujenzi wa madarasa hayo umetokana na fedha zaidi ya Sh.bilioni tatu ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni mkakati wake wa kutatua changamoto ya upungufu wa madarasa katika Shule sa sekondari
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa tukio la Makabidhiano ya madarasa 157 ya shule za sekondari katika Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.Fedha za ujenzi wa madarasa hayo ambazo ni zaidi ya Sh.bilioni tatu zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...